WAPIGA DEBE WAENDELEA KUKAIDI AGIZO STEND KUU SENGEREMA
Kufuatia baadhi wa Wapiga
debe kuendelea kukaidi agizo lilitolewa na serikali la kuondoka katika stend
kuu ya Magari mjini Sengerema Afisa Usalama barabarani wilayani Sengerema
Inspecta Hamis Wembo amewataka kuondoka mara moja.
Insepcta Wembo ameyasema
hayo wakati akizungumza na Radio Sengerema ambapo amesema mpaka sasa baadhi ya
wapiga debe wamekamatwa kwa kushindwa kutii agizo hilo na tayari wamefikishwa
mahakamani.
Afisa usalama
barabarani amewataka wapiga debe hao waangalie
njia nyingine ya kutafuta riziki katika maisha
na kwamba wakiwa wahalifu watachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wao wapiga
debe wamesema kuwa agizo hilo linawaumiza na kuiomba serikali iwaangalie kwa
mara ya pili kwani hawana sehemu ya kwenda.
Hata hivyo inspekta
Wembo amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kupambana na wale wote watakaovunja
utaratibu uliowekwa,na kwamba zoezi hili sio
kwa Wilaya ya Sengerema pekee yake
bali ni kwa Taifa zima.
Na Glorius Balele.
Comments
Post a Comment