ELIMU KWA WAFUGAJI WA KUKU SENGEREMA.
Wafugaji wa
kuku wilayani Sengerema
wametakiwa kuwapatia chanjo
kuku wao
kwa kufuata maelekezo
sahihi kutoka kwa
watalamu wa mifugo .
Hayo yamebainishwa
na mwezeshaji wa shirika
la Farmers Empowerment Intietive (FEI ) linalojihusisha na
utoaji elimu kwa wakulima na wafugaji
ambae
pia ni afisa
mifugo wilaya ya Sengerema bwana
GEORGE NKUBA ,katika
mkuutano uliofanyika katika
ukumbi wa kituo cha habari
na mawasiliano Sengerema
Telesentre na kusema kuwa
lengo la kuendesha semina hiyo ni kuwasaidia wafugaji waweze kutumia mfumo mzuri wa ufugaji na usio hitaji mtaji mkubwa.
Hata hivyo
bwana NKUBA amewataka wafugaji wa kuku
kuwapatia chanjo kuku wao kwa kufuata maelekezo
wanayopewa na watalaamu
ili kuondokana na
magonjwa yasio ya
lazima kwa mifugo.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa
shirika hilo la
FEI bwana ,ZEPHANIA LUTOBEKA
amesema kuwa lengo la
shirika hilo ni
kumwezesha mkulima na
mfugaji kumpa uwezo
wa kilimo
.
Kwa upande
wake wadau wa shirika
hilo wamelipongeza shirika
hilo kwa kuwaelimisha juu ya
ufugaji wa kuku
pamoja na uendeshaji wa
kilimo .
Aidha katika
hatua nyingine wafugaji
wameaswa kuacha kutumia
maji ya bomba wakati
wa kuchanganya dawa
ya kuku wao.
.
Na, Enosy Mashiba.
Comments
Post a Comment