VITENDO VYA KIHALIFU VYAWATESA ILEKANILO SENGEREMA
Wananchi wa kijiji
cha Ilekanilo kata ya Kasungamile wilayani Sengerema mkoani
Mwanza wamekubaliana kufanya ulinzi
shirikishi ili kudhibiti matukio
ya uhalifu kijijini hapo.
Makubaliano hayo
yamefanyika kwenye kikao cha kubaini wahalifu kufuatia tukio la ujambazi
lililofanyika kijijini hapo kwa pamoja wameweka mikakati ya ulinzi ili
kuhakikisha tukio hilo halitokei tena.
Akizungumza kwenye
mkutano huo mwenyekiti wa kijiji cha Ilekanilo
Bwana Fikiri Yakobo Ruhusa
amewataka wananchi kuwa na subira na kushirikiana katika kutokomeza matukio ya
ujambazi
Naye Diwani wa kata ya
Kasungamile Mh,Julias Ndekeja
amekubaliana na upigaji wa kura za siri ili kuwabaini watu wanaosumbua kwa
matukio ya uhalifu pia amewataka wananchi kushikamana katika kupambana na
matukio ya uhalifu.
Ndekeja amesema kutokana na matukio ya ujambazi
kuongezeka katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krismassi na mwaka mpya
wananchi wametakiwa kuongeza umakini kwa wageni mara wanapoona au kusikia
jambo linaloweza kuleta uvunjifu wa
amani kutoa taarifa kwa viongozi.
Na Charles Sungura.
Comments
Post a Comment