KANISA LA GMC LAZUA KIZAA ZAA SENGEREMA

Mwenyekiti  wa  mtaa  wa  maduka  matatu  kata  ya  Nyatukara  wilayani  Sengerema   bwana   PASCHAL     LUJIGILWA,  amelionya   vikali   kanisa  la  GMC  liliopo   katika   mtaa   huo   kwa   madai   ya   utovu  wa  nidhamu.

Mwenyekiti  huyo  ametoa  kauli  hiyo  katika  mukutano  wa  hadhara  uliofanyika  katika   mtaa  huo    na  kusema  kuwa  wameshindwa  kuwaheshimu  wananchi  wa  eneo  hilo  wakati  wakiwa  wanafanya  mkuutano  huku  wao  wakiwa  wanaendelea  kufanya  mazoezi  ya  kwaya  hali   iliyopelekea   kushindwa  kuelewana  katika  mkuutano  huo.

Katika  hatua  nyingine  wananchi  wa  eneo  hilo  wamekerwa   na   tabia   kwani  limekuwa  ni  tatizo   la  mda  mrefu   mpaka   sasa  huku  wengi  wao  wakimpongeza   mwenyekiti  wa  mtaa  huo  kwa  hatua   aliyoichukuwa  ya   kuwaonywa  kwani  pengine  itakuwa  ni  suluhisho   la  kudumu.


Hata  hivyo   kwa  upande  wake   mama  mchungaji  wa  kanisa  hilo  la  GMC   ambaye  hakujitambulisha  kwa  jina  amekiri  kuwepo  kwa  kitendo  hicho  huku  akiomba  msamaha  mbele  ya  mkuutano huo  na  kudai  kuwa  tatizo  hilo  halitajirudia  tena.
Na Enosy Mashiba

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA