AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KISA UBAKAJI WA MTOTO WA MIAKA 7 SENGEREMA
Mtu mmoja amefikishwa
katika mahakama ya wilaya ya Sengerema Mkoani
Mwanza kwa tuhuma ya ubakaji.
Mbele ya hakimu mkazi
wa mahakama hiyo Monica Ndyekobora mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi
insipekta Sylivester Mwaiseje amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Robert Pamo mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa Nyamililo
wilayani Sengerema mkoani humo.
Mwaiseje amesema
mtuhumiwa ametenda kosa hilo November 11 mwaka huu majira ya saa 4 katika
kijiji cha kijiweni kilichopo wilayani Sengerema ambapo alimbaka mtoto ambaye jina lake limehifadhiwa
mwenye umri wa miaka saba.
Mtuhumiwa ametenda kosa
hilo kinyume na kifungu cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na chapili{e} na kifungu cha 131 kifungu kidogo cha kwanza cha
kanuni ya adhabu.
Mshitakiwa
amekiri kosa pamoja na maelezo ya awali ya kosa hilo na amehukumiwa kutumikia
kifungo cha miaka thelathini 30 jela.
Na HAPPYNESS PAUL
Comments
Post a Comment