UNDP YAWASILISHA RIPORT YA MAJARIBIO YA AWALI YA MRADI WA UZALISHAJI GESI ASILIA HALMASHAURI YA SENGEREMA
Majaribio ya awali ya Mradi wa uzalishaji wa Gesi
asilia kupitia ufadhiri wa
shirika la United Nations
Development Programme (UNDP) umeonekana
kuwa na mafanikio makubwa kwa
jamii ya wilaya
ya Sengerema kutokana
kupunguza
tatizo
la kukata miti ovyo
na kupunguza
uharibifu wa Mazingira.
TIMU KUTOKA UNDP PAMOJA NA WATAALAM WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUWASILISHA RIPORT YA MAJARIBIO YA AWALI YA MRADI WA UZALISHAJI WA GESI ASILIA KATIKA HALMASHAURI YA SENGEREMA. |
Mradi huo
umeingia wilayani Sengerema
mnamo mwaka 2015
katika kijiji cha
Nyampande wilayani hapa
ambapo umeonekana kuwa
na mwitikio mkubwa
kwa jamii kuhitaji kutumia
mradi huo.
Akizungumzia mradi
huo mwezeshaji wa
mradi UNDP Joseph Malkia kwa
niaba ya shirika
la UNDP ameeleza jinsi
jamii ilivyoupokea mradi
huo.
Kwa upande
wake Afisa mazingira
wa wilaya
ya Sengerema Bwn, Ally
Salim amefafanua mfumo
wa mradi huo
unavyofanya katika jamii .
Aidha Bwn,
Salim ameongeza kuwa
baada ya mradi
huo kuanza wamejitahidi
kutoa elimu juu
ya faida ya
mradi kwa jamii
na kuwahidi kuwa kupitia
mradi huo watalinda mazingira
pamoja na kuwapa
watoto na kinamama
nafasi ya kuachana
na utafutaji wa
kuni.
Na Thobias Ngubila.
Comments
Post a Comment