MBWA WAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA SENGEREMA
Mama
mmoja aliyejulikana kwa jina la Martina
John anaekadiliwa kuwa na umri wa
miaka 50 ameng’atwa na mbwa na kumjeruhi goti la mguu wa kushoto katika kata ya
mwabaruhi wilayani Sengerema.
Akiongea
na Radio Sengerema mama huyo amesema kuwa alikuwa akipita njiani akielekea
shambani ndipo mbwa waliokuwa kwenye mji walimkimbia na kuanza kumshambulia.
Radio
senerema imemtafuta mmiliki wa mbwa hao Bi.EVA PHILIMON amekiri mbwa wake kumng’ata mama huyo na
ameahidi kumpeleka katika huduma za matibabu.
Awali
balozi wa mtaa wa Kanyamwanza bw.SIMON
MPUYA amekuwa akiwatahadharisha wamiliki wa mbwa kuwafungia nyakati za mchana
licha ya baadhi yao kuendelea kukiuka maagizo hayo.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Kanyamwanza bw.INNOCENT SEGEREDI amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo huku akiwaasa wamiliki wa mbwa kuwafungia ndani ya kibanda nyakati za
mchana ili kunusuru matukio ya mbwa kuwashambulia watu.
Na Anna Elias
Comments
Post a Comment