MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA AIPONGEZA RADIO SENGEREMA
Kutokana na vipindi
mbalimbali vya kuelimisha jamii vinavyoruka kupitia kituo cha habari na
mawasiliano Sengerema Telecenter Mkuu wa
wilaya ya Sengerema Mh Emmanuel Kipole
amewashukuru watumishi wa wa kituo hiki
kwa kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi juu ya haki ya mtuhumiwa awapo
katika vyombo vya dola wilayani Sengerema.
Mh Kipole amewashukuru watumishi hao kupitia makala ya Jicho la jamii
inayorushwa na Radio Sengerema na kudai kuwa kipindi hicho kimekuwa kikitoa
elimu kwa jamii husika hivyo wananchi wazingatie elimu hiyo kwani ina manufaa
kwao.
Aidha amewataka raia
kutambua kuwa mtu yeyote anapaswa kuzitambua haki zake pindi anapokuwa katika
vyombo vya dola na kuongeza kuwa kutuhumiwa ni jambo la kila mtu hivyo
wazingatie ni hatua zipi zinazotakiwa kuchukuliwa na sio kuwabishia askari
pindi wanapowakamata wakidai kutenda kosa.
Mh,Kipole amewaomba wananchi wanaoishi vijiji kuacha
kutetereka pindi wanapotuhumiwa kutenda
kosa kwani mtuhumiwa yeyote anawajibu wa kujieleza mbele ya vyombo vya dola.
Sanjari na hayo ametoa rai kwa baadhi ya askari wenye tabia ya
kuwanyanyasa watuhumiwa pindi wanapowafikisha katika jeshi la polisi.
Na Enock Makala
Comments
Post a Comment