TISHIO LA FISI GEITA AJERUHI WATU 3
Watu watatu wameshambuliwa
na fisi na kujeruhiwa sehemu
mbalimbali za miili yao katika kijiji
cha Idoselo Kata ya Lwezela Mkoani Geita .
Afisa mtendaji wa
kijiji cha Idoselo Bwn Samson Kachimu Walwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa kundi la fisi hao wamevamia katika baadhi ya familia
mkoani humo kwa lengo la kutafuta
mbuzi ndipo watu hao waliposhambuliwa na
fisi hao.
Bwn,Walwa amesema kuwa
majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Mkoa
wa Geita kwa matibabu zaidi.
Na Emmanuel Twimanye
Comments
Post a Comment