MJI WA SENGEREMA WAANZA KUIMARIKA KWA USAFI

Hatimae mji wa Sengerema umeonekana kuwa katika hali ya usafi kutokana na kampuni iliyokabidhiwa kufanya kazi hiyo kuzoa  taka kwa wakati kwa baadhi ya maeneo mjini hapa.
Wafanya usafi wakifanya usafi mjini Sengerema


Taka hizo zimeonekana kupungua kutokana na kampuni iliyo kuwepo kushindwa kufanya kazi hiyo ,na kukabidhiwa Kampuni ya mazingira ya  Social  Environmental Workers Association (SEWA) ambayo imeonekana kuwa na kasi zaidi katika shuguli hiyo.

Akitolea ufafanuzi  wa maeneo ambayo hayajafikiwa kwa wakati, mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bwn.Ndaturu Yohana amesema sababu kubwa ni kutokana na upungufu wa vitendea kazi, na kuwaomba wananchi  kuwa na subira kwani  ndani ya muda usiozidi siku 14 maeneo yote yatakuwa katika hali ya usafi mjini Sengerema.

Aidha baadhi ya wananchi wamewaomba  wafanyausafi hao kuwafikia katika maeneo yalio nje ya mji ,hususani katika msimu huu wa masika.


Vilevile Bwn.Yohana  amewaomba wananchi kila moja kuujua umuhimu wa kutunza mazingira.

Na Esther Mabula.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA