SIKU 2 ZATOLEWA KWA WAPIGA DEBE KUONDOKA STENDI MJINI SENGEREMA
Jeshi la polisi kitengo
cha usalama barabarani Wilayani Sengerema
limetoa muda wa siku mbili
kwa
wapiga debe waliopo katika kituo
kikuu cha mabasi wilaya Sengerema kuondoka mara moja
na atakaye kiuka agizo hilo atachukuliwa hatua
kali za kisheria.
Hayo yamesemwa na mkuu
wa kitengo cha usalama barabarani Insipecta
Hamis Wembo ambapo amesema agizo hilo ni
maelekezo yaliyotolewa kutoka
ngazi ya juu ya serikali kuwa kuwepo kwa wapiga debe wengi ni chanzo cha
usumbufu kwa abiria na kwamba maelekezo hayo yasipo fanyiwa kazi hatua za
kisheria zitachukuliwa.
Kwa upande wao baadhi
ya wapiga debe wamelipokea agizo hilo vizuri na kuahidi
kuwa watalifanyia kazi kama
walivyo agizwa ,huku wengine wakilipokea kinyonge kutokana na kwamba sehemu hiyo ilikuwa ni moja ya kujipatia riziki
katika maisha yao.
Sambamba na hayo
inspector Wembo amesisitiza suala la usalama barabarani kwa kuwataka madereva wa vyombo vya moto makini
wawapo safarini ili kuepusha ajali za barabarani ikiwemo
kuzingatia sheria na alama zilizowekwa
barabarani.
Na, Glorius Balele
Comments
Post a Comment