KIAMA CHATANGAZWA KWA WANAOAJIRI WATOTO CHINI YA MIAKA 18
Wananchi wanaowajiri
watoto kufanya kazi za ndani wametakiwa kuzijua sheri za watoto kabla ya kuwapatia
ajira na kuhakikisha kazi wanazowapa
haziwadhuru kiafya, kielimu na katika ukuaji wao.
Hayo yamebainishwa na
Afisa ustawi wa jamii wilayani sengerema
mkaoani mwanza Nyanjige Julius Nkwabi
wakati akizungumza na Redio Sengerema.
Afisa ustawi amesema
kuwa wanapaswa kutambua kuwa wanapoajiri mtoto aliyechini
ya umri wa miaka 18 watambue kuwa huyo ni mtoto na alindwe kwa mujibu wa
sheria.
Hata hivyo amewataka watoto pamoja na wazazi wa
watoto hao kutoa taarifa katika ofisi za ustawi wa jamii ama ofisi za
serikali za mitaa pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili .
Na Neema Hussin.
Comments
Post a Comment