RADIO SENGEREMA YAWASAIDIA WAJASILIAMALI WALIOTISHIWA KUONDOLEWA GEITA
Wajasiliamali wanaojishughulisha na upondaji kokoto katika mlima uliopo eneo
la IBanda kata ya Kanyala wilayani Geita mkoani Geita wameipongeza Radio Sengerema
kwa kuwasaidia kuendelea kufanya kazi
katika mlima huo licha ya viongozi wa
eneo hilo kutaka kuwaondoa.
Pongezi hizo wamezitoa
wakati Radio Sengerema ilipotembelea katika mlima huo kwa lengo la kujua kama
shughuli zinaendelea za upondaji kokoto kwa wajasiliamali hao.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa wajasiliamali wa eneo hilo a nae ameipongeza Radio Sengerema kwa kufanikisha
kumaliza mgogoro huo baina ya wajasiliamali na viongozi wa
eneo hilo.
Mwaka jana viongozi wa
eneo la Ibanda walilazimika kuitisha mkutano kwa lengo la kuwahamisha
wajasiliamali hao kwa kigezo cha kupata mwekezaji ambaye alihitaji kuwekeza
katika mlima huo.
Na Said Mahera.
Comments
Post a Comment