JAMII YAHIMIZWA KUSAFISHA MAZINGIRA SENGEREMA
Wananchi wametakiwa
kuzingatia suala la usafi wa mazingira na kuachana na dhana ya kusubiri kusukumwa
na viongozi ili kuepusha magonjwa ya mlipuko
katika kipindi hiki cha mvua.
Hayo yamebainishwa na
Mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Kata ya
Nyampulukano wilayani sengerema,Bwn Goodluck
Daud wakati akizungumza na Radio Sengerema ofisini kwake.
Bwn,Daud
ameongeza kuwa,kipindi hiki cha mvua ni hatarishi kwani kuna uwezekano mkubwa
wakutokea magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Pia amewataka wananchi
kulinda na kuishi katika hali ya usafi ili waimalishe afya za familia kwa
ujumla.
Hata hivyo,amefafanua
kuwa jamii imekuwa na mwitikio mkubwa katika suala nzima la usafi na wanaokaidi
hufikishwa katika vyomba vya sheria kwa hatua zaidi.
Na Michael Mgozi
Comments
Post a Comment