WANANCHI WABORESHA HUDUMA ZA MAJI Wananchi wa Kitongoji cha Kanyamwanza kata ya Mwabaluhi wilaya ya sengerema mkoani mwanza wamepongezwa kwa juhudi za kuboresha huduma ya maji kwa kuvuta mabomba ya maji katika kitongoji chao. Pongezo hizo zimetolewa na mwenyekiti wa kitongoji cha kanyamwanza bwana INNOCENT SEGEREDI wakati akizungumza na wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji hicho ambapo amewambia wananchi wake hawana budi kujipongeza kwa juhudi walizozifanya za kusogeza maji karibu na makazi yao. Bwana INNOCENT amewaasa wananchi wake wanaohitaji kuvuta maji waweze kuchangia kiasi cha fedha walichokubaliana katika mitaa yao ili waweze kupata maji na wasitegemee kula kwa nguvu za wenzao. Pamoja na hayo mwenyekiti huyo amewaomba wakazi wa eneo hilo waendelee kuyatunza mazingira yanayowazunguka hasa kwa kipindi hiki cha mvua. NA ENOCK MAKALA
Posts
Showing posts from October, 2017
- Get link
- X
- Other Apps
WAFANYAUSAFI WASITISHA MGOMO WAO WALIPWA STAHIKI ZAO SENGEREMA Hatimae vizimba vya taka vilivyokuwa vimejaa kwa zaidi ya wiki mbili bila kuondolewa taka na kusababisha kero kwa wakazi wa mji wa sengerema,vimeanza kuondolewa baada ya wahusika kumaliza mgomo wao. Akizungumza na Radio sengerema meneja wa kampuni ya Stumarcot Company Limited Bwn CHARLES NGAIZA, amesema,uchafu ulikuwa umejaa kutokana na mgomo wa wafanyakazi wa kampuni hiyo. Aidha Bwn NGAIZA ameongeza kuwa,toka tarehe moja mwezi huu, wafanyakazi walikuwa wamegoma na kusababisha mlundikano wa taka katika vizimba vyote vya mji wa sengerema. Sanjari na hayo kiongozi huyo amesema,watatumia wiki moja kuhakikisha wanamaliza kuondoa uchafu huo, na kwa sasa wameanzia madampo yaliyopo katikati mwa mji wa sengerema hususani maeneo ya kituo cha mabasi sengerema, Na Michael Mgozi
- Get link
- X
- Other Apps
MWENYEKITI ATOA ELIMU YA VITAMBULISHO VYA NIDA Mwenyekiti wa kitongoji cha kanyamwanza kata ya mwabuluhi wilaya ya sengerema mkoani mwanza bwana Innocent Segeredi ametoa elimu juu ya uandikishaji wa vitambulisho vya uraia (NIDA). Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji hicho bwana Segeredi amewafafanulia kwa undani juu ya kitambulisho cha uraia na kuwaelezea jinsi gani ya kujaza fomu ya maombi ya utambulisho. Aidha mwenyekiti huyo amewataka wananchi waendelee kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika mazingira yao hasa kipindi hiki cha mvua. Pamoja na hayo Bwana Segeredi amewaomba wananchi wa mtaa wake kutii suala hilo la kujiandikisha kwani vitambulisho vya uraia ni muhimu. Na Enock Makala
- Get link
- X
- Other Apps
WAFANYA USAFI WAGOMA MJINI SENGEREMA Wafanyausafi mjini Sengerema wamegoma kuendelea kufanya usafi kwa takribani wiki mbili sasa kutokana na kutolipwa stahiki zao kwa muda mrefu. Wafanyausafi hao wamedai kuwa kumekuwa na tatizo la kutopewa mishahara yao kwa wakati hali ambayo imekuwa ikikwamisha zoezi zima la usafishaji wa mji kwa wakati. Akijibu madai hayo Meneja wa kampuni ya Stumarcot Company Limited amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kuongeza kuwa madai ya mishahara kwa wafanyausafi hao yamechukuwa muda mrefu na kwamba suala hilo wameanza kulitatua. Aidha tatizo hilo la ktolipwa stahiki zao kwa wakati limesababisha wafanyausafi kukata tamaa kuendelea na kazi hiyo kwa kuhofia kukosa maslahi yao. Na Thobias Ngubila
- Get link
- X
- Other Apps
WITO WA JAMII Wazazi wametakiwa kuwalea watoto kiroho na kimwili ili wawe na tabia njema ya kumpendeza mwenyezi mungu katika maisha yao. Wito huo umetolewa na mchungaji wa kanisa la Africa inland church of Tanzania (A.I.C.T) Pastoreti ya Nyamililo Kata ya kasungamile wilayani Sengerema mkoani Mwanza Mchungaji Adamu Loke Mabindo kwenye sherehe ya kukabidhi biblia na vyeti kwa watoto waliohitimu mafunzo ya neno la mungu. Mchungaji Mabindo amesema msingi imara wa maisha kwa watoto ni kuwafundisha neno la mungu ili wamjue mungu na kisha elimu ya dunia ambayo itawasaidia kimwili. Aidha mchungaji huyo ameyashukuru mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mwanza children Action Network na shirika la samalatans Purse kitengo cha O.C.C kwa kutoa biblia na vyeti kwa watoto. Mchungaji Mabindo ameahidi kuendelea kushirikiana mashirika hayo ili kuboresha darasa la watoto. Mchungaji amewaomba wananchi kuungana kwa pamoja katika malezi ya watoto kwakuwa jukumu la kuwalea watoto katika
- Get link
- X
- Other Apps
MKUU WA SHULE ALIYEJINYONGA AZIKWA Mwili wa aliyekuwa mkuu wa shule ya Sekondari Migukulama iliyopo katika kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema hatimaye umezikwa nyumbani kwao katika kata ya Kasisa halmashauri ya Buchosa. Mazishi hayo yameongozwa na Mkurugezi Mtendaji wa halmashauri ya Buchosa Bwana Crispin Luanda ambaye amewakilishwa na Afisa elimu shule za Msingi Bi, Magreti Kapolesya. Bi. Kapolesya akitoa salamu za rambirambi kwa wana familia na wanachi wa kijiji hicho amesema serikali imepoteza nguvu kazi kwani bado umli wake ulihitajika kulitumikia taifa Ikumbukwe kuwa mkuu wa shule ya sekondari Migukulama Benedictor Rweikiza (45) Octoba 9 mwaka huu alikutwa akiwa amefariki dunia kwakujinyonga kwa kutumia kamba nyumbani kwake katika mtaa wa kilabela kata ya Nyatukala wilayani Sengerema. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo watumishi wa halmashauri ya Buchosa,Mbunge wa jimbo la Buchosa,wakuu wa shule jirani madiwani
- Get link
- X
- Other Apps
UCHAFUZI KANDO KANDO MWA ZIWA VICTORIA Wananchi wa Kijiji cha Nyakaliro Kata ya Nyakaliro Halimashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kuacha kukata miti kandokando mwa ziwa victoria ili kulinda mazalia ya samaki,na kuepusha mmomonyoko wa udongo unaoweza kujitokeza. Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyakaliro Bwn MAGAKA SITTA,wakati akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake. Bwn SITTA Amesema kuwa ,wakati mwingine samaki huzalia kandokando ya ziwa,wanapokata miti na sehemu hiyo kubaki wazi, hali hiyo huchangia kuondoa viumbe hai wanaokuwa na makazi katika maeneo hayo. Hata hivyo ameongeza kuwa zipo sheria ndogondogo walizo weka ili kulinda vyanzo vya maji pamoja na uhifadhi wa mazingira kandokando mwa vyanzo vya maji na ziwa kwa ujumla. misitu. Na Michael Mgozi
- Get link
- X
- Other Apps
MADEREVA WANAOBEBA MISHIKAKI KUKIONA CHA MOTO kikosi cha usalama barabarani kimewatangazia vita madereva wanaobeba abiria zaidi ya mmoja hususani wanaosafirisha abiria kwenda vijijini. Vita hiyo imetangazwa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Inspector Hamis Wembo wakati alipokuwa akiongea na Radio Sengerema amesema kwa maeneo ya vijijini wameelekeza majeshi ili kuhakikisha badereva ambao hawatii sheria bila shuruti wanakamatwa na kufikishwa mahakamani. Inspector Hamis Wembo ameeleza mikakati ambayo kikosi cha usalama barabarani watakayoitumia ili kuakikisha wanawakamata waendesha bodaboda ambao watakaobeba abiria zaidi ya mmoja. Katika hatua nyingine Inspector wembo amewaomba madereva kuzingatia uvaaji wa kofia ngumu kwa abiria kwani ni kwaajiri ya usalama wa maisha yao. Na Said Mahera
- Get link
- X
- Other Apps
NYAVU 78 ZAKAMATWA HALMASHAURI YA BUCHOSA Jumla ya nyavu haramu 78 zenye thamani ya sh.milion tatu laki moja na ishirini zimekamatwa katika kata ya Bulyaheke wilayani Sengerema Mkoani Mwanza. Zoezi la kukamata nyavu hizo limeongozwa na Afisa Mtendaji wa kata ya Bulyaheke Mussa Mwilomba kwa kushirikiana na wananchi. Hata hivyo Afisa Mtendaji amesema walipata taarifa kutoka kwa raia wema ndipo waliopoanza msako katika kijiji cha Mbungani eneo la Chiloloma ndipo walifanikiwa kukamata nyavu 78 katika eneo hilo. Aidha ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana kwa pamoja ili kukomesha uvuvi haramu Na Deborah Maisa
- Get link
- X
- Other Apps
WANANCHI WAJITOLEA KUKARABATI BARABARA ZA MITAA Wananchi wa mtaa wa Kilabela kata ya Mwabaluhi wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wameamua kushirikiana kwa pamoja kukarabati barabara za mtaa huo ili kupunguza adha wanayoipata wakati kusafirisha mazao pamoja na wagonjwa. Wananchi hao wameeleza kuwa ushirikiano huo umesaidia kuwepo kwa barabara za kutosha zinazopitika kwa urahisi hali ambayo wameeleza kuwa inasaidia kuongeza maendeleo katika mtaa huo. Akizungumza na Radio Sengerema ofisini kwake , Mwenyekiti wa mtaa huo bw, Samweli Macheni Nzungu amesema wananchi wake wanaonyesha mshikamano mzuri wa shughuli mbali mbali za kimaendeleo. Sanjari na hayo bw, Nzungu amewasihi wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili wasonge mbele zaidi. Na Thobias Ngubila
- Get link
- X
- Other Apps
UVAMIZI WAFANYIKA SENGEREMA Kutokana na Kudhibitiwa vikali matukio mbalimbali ya uporaji wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, kwa sasa yameibuka tena kwa sura mpya katika kata ya Mwabaluhi kitongoji cha Kanyamwanza wilayani Sengerema, baada ya kuvamiwa familia ya Mzee Joseph Maganga na kuiba vitu mbalimbali. Tukio hilo limetokea katika eneo hilo ambapo watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi hao wamefanikiwa kupora vitu ikiwemo frati skilini 1 Deki 1 na simu 3 za mkononi vyenye Thamani ya shilingi milioni moja na laki nne na nusu, na kutokomea navyo kusikojulikana . Imeelezwa kuwa watu hao wametumia ufunguo maarufu kama masta kii kufunguwa mlango wa geti na baada ya kufungua geti hilo wakapiga fatuma mlango wa ndani na kufunguka ndipo walipoingia na kuanza zoezi la upekuzi na kubeba mali hizo. Kwaupande wake mwenye kiti wa mtaa wa eneo la Kanyamwanza kulikofanyika wizi huo Bw,Peter Mlashani, amethibitisha kut
- Get link
- X
- Other Apps
WANANCHI WAJENGEWA DARAJA Wananchi wamepongeza juhudi za serikali kwa kujenga daraja la Bulunga katika kijiji cha Nyamililo kata ya Kasungamile wilayani Sengerema na kumaliza kero ya muda mrefu ya kuvuka mto huo. Wakizungumza na Radio Sengerema kijijini hapo wamesema pamoja na pongezi hizo wameitaka Serikali kuboresha miundo mbinu ya barabara hiyo kutoka Nyamililo kwenda Bulunga ambalo ni bovu na halipitiki. Naye Diwani wa kata ya Kasungamile mh: Julias Ndekeja amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali ikijiandaa kukarabati barabara hiyo. Kukamilika kwa daraja la Nyamililo kwenda Bulunga kumewafanya wananchi kuwa na matumaini makubwa na juhudi za serikali katika utekelezaji wa ahadi zake. Na Charles Sungura
- Get link
- X
- Other Apps
KAMPENI YA PAZA SAUTI ABIRIA YAFANIKIWA KWA ASILIMIA 75 Abiria wametakiwa kupaza sauti pindi wanapoona dereva amekwenda kinyume na sheria za usalama barabarani na siyo kulalamika bila kuchukua hatua ili kuepuka kuhatarisha maisha yao. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa elimu kwa umma kitengo cha usalama barabarani Wilayani Sengerema Coplo Echikaka Mbozi wakati akichangia maoni katika kipindi cha Pambazuko kilichokuwa kikihoji Kampeni ya pasa sauti abiria imefanikiwa kwa kiasi gani? Akijibu hoja hiyo Coplo Echikaka Mbozi amesema kampeni hiyo imefanikiwa kwa asilimia 75 nchini na kuwataka abiria watoe taarifa kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani pale wanapoona dereva amekwenda kinyume na sheria za usalama barabarani kwani kulalamika hakutawasaidia . Na Emmanuel Twimanye
- Get link
- X
- Other Apps
WANAFUNZI 2,262VYUMBA VYA MADARASA SITA SHULE YA MSINGI MNADANI. Kutokana na kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi mnadani iliyopo kata ya Nyampulukano wilayani sengerema tatizo hilo limeanza kupatiwa ufumbuzi . Hayo yamebainishwa na Afisa mtendaji wa kata ya Nyampulukano BI. SOPHIA MANYILIZU na kusema kuwa shule ya msingi mnadani ina jumla ya wanafunzi 2262 huku ikiwa na vyumba vya madasa sita hali ambayo inapelekea baadhi ya wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao. Hata hivyo diwani wa kata ya Nyampulukano Mh,Emmanuel Zacharia Mnwanizi amesema wanahitaji kuongeza madarasa manne ili kupunguza adha iliyopo ya uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo. Aidha diwani mnwanizi amewaomba wadau mbalimbali kujitolea nguvu zao ili kuhakikisha kwamba ujenzi wa vyumba vya madarsa unaanza mara moja. Na Enosy
- Get link
- X
- Other Apps
UTUNZAJI WA MAZINGIRA Jamii imetakiwa kutunza mazingira kwa kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo cha kudumu ili kuepusha uharibifu wa mazingira katika maeneo yao. Hayo yamesemwa na afisa afya wa kata ya Igalula Bwn;Emmanuel Saguda katika kikao na wananchi wa kijiji cha Nyasigu kata ya Igalula wilayani Sengerema, ambapo amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi watu kusubiria ukaguzi ndipo wanatengeneza vyoo vya muda ili kujikinga na ukaguzi huo. Kwa upande wake Diwani wa kata ya Igalula Mh, Onesmo Mussa Mashiri amewaomba wananchi wote kunzingatia yanayo semwa na wataalamu kwa kutunza mazingira. Hata hivyo maeneo mengi ya vijijini yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya ukataji miti ovyo, uhaba wa vyoo hivyo kupelekea wananchi kujisaidia vichakani jambo ambalo siyo salama kwa afya zao.
- Get link
- X
- Other Apps
ANUSURIKA KIFO KISA PIKI PIKI Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Leila Mangi Mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Igogo Wilayani Sengerema amenusurika kifo baada ya kugongwa na pikipiki mjini sengerema Mkoani Mwanza. Ajali hiyo imetokea katika barabara iendayo Kamanga baada ya mwendesha Pikipiki kupishana na gari aina ya fuso na kumgonga mtembea kwa miguu Leila Mangi na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake. Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Inspector Hamis Wembo amewaomba waendesha vyombo vya moto kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo kusudiwa. Jeshi la polisi limefika eneo la tukio na kumchukua majeruhi kisha kumpeleka katika Hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Na Said Mahera
- Get link
- X
- Other Apps
ELIMU BURE ISIMAMIWE IPASAVYO Kutokana na serikali kutumia zaidi ya shillingi bilion 18 kugharamia utekelezaji wa sera ya elimu bure viongozi wa ngazi ya kata katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema wametakiwa kusimamia na kuhakikisha wanafunzi wote waliohitmu elimu ya msingi wanajiunga na masomo ya sekondari pindi watakapochaguliwa. Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Sengerema Bwn, Aron Laiza amesema serikali ngazi ya kata,kijiji inatakiwa kusimamia wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza. Pia ameongeza kuwa kwa mzazi yeyote atakabainika kumzuia mtoto kwenda shule hatua kali zitachukuliwa na viongozi dhidi yake. Hata hivyo utekelezaji wa sera ya elimu bure unalenga kutoa fursa ya elimu kwa watoto wote nchini ili kila mmoja aweze kupata haki yake ya msingi ya elimu. Na Deborah Maisa
- Get link
- X
- Other Apps
HUDUMA YA MAJI YAREJEA SENGEREMA Shangwe na ndelemo zimetawala Kwa Wananchi Wilayani Sengerema baada ya kurejea huduma ya maji iliyokuwa imekatika kwa takribani wiki mbili sasa. Wakiongea na Radio Sengerema wananchi hao wamesema maji yameanza kutoka usiku wa kuanzia leo huku wakisema imekuwa shangwe kwao kwani walikuwa wakihofia kupatwa na magonjwa ya mlipuko na kushukuru uongozi wa wilaya ya Sengerema kwa jitihada za kurejesha huduma hiyo muhimu. Hata hivyo pamoja na pongezi hizo wananchi hao wameomba uongozi wa halmashauri kuendelea kufuatilia deni hilo kama alivyosema mkuu wa wilaya Mh.Emmanuel Kipole ili katizo la maji lisijirudie tena. Na Anna Elias
- Get link
- X
- Other Apps
JAMII YATAKIWA KUIMALISHA ULINZI Jamii imetakiwa kuimalisha ulinzi katika maeneo yao ili kupambana na vitendo vya kihalifu vinavyoendelea kujitokeza katika maeneo mengi, kwani suala la ulinzi ni wajibu wa kila mtu. Taarifa na Mwandishi wetu MICHAEL MGOZI. Hayo yamebainishwa na Afisa mtendaji wa kata ya Ibisabageni Bwn,Adam Salum wakati akizungumza na Radio Sengerema Ofsini kwake. Bwn, Adam ameongeza kuwa jamii inapaswa kutambua suala la ulinzi na kulisimamia vyema,kwani ni wajibu wao kuwafichua wahalifu wanaoishi katika maeneo yao. Aidha Afisa Mtendaji huyo amewataka wanachi kuwabaini wahalifu mapema kabla hawajafanya uhalifu na kuacha tabia ya kusubiri tukio la kihalifu pindi linapotokea ndipo wanaanza kuimalisha ulinzi. Na Michael Mgozi.
- Get link
- X
- Other Apps
KATIZO LA MAJI LAWATESA WAKAZI WA SENGEREMA Emmanuel Kipole Kutokana na kuwepo kwa tatizo la kukatika kwa huduma ya maji mjini Sengerema kwa takribani wiki mbili sasa bila taarifa yoyote kutoka mamlaka husika ya maji, Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Emmanuel Kipole ametolea ufafanuzi wa kina suala hilo . Akitilitolea ufafanuzi jambo hilo mkuu wa wilaya ya Sengerema ameiambia Radio Sengerema kuwa tatizo hilo limetokana na deni waliokuwa wakidaiwa siku za nyuma na shirika la umeme Tanzania (TANESCO) zaidi ya milioni 200 hali iliyopekea kukatiwa umeme katika chanzo cha maji cha Nyamazugo. Mh,KIPOLE Amesema juhudi zinafanyika ili kutatua tatizo hilo huku akiwaomba radhi wananchi kwa adha wanayoipata ya ukosefu wa huduma ya maji. Aidha amewaomba wananchi waendelee kulipa bili ya maji ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza. Na Anna Elias