KAMPENI YA PAZA
SAUTI ABIRIA YAFANIKIWA KWA ASILIMIA 75
Abiria wametakiwa
kupaza sauti
pindi wanapoona dereva amekwenda kinyume
na sheria za usalama
barabarani na siyo
kulalamika bila kuchukua hatua ili kuepuka kuhatarisha maisha yao.
Kauli hiyo
imetolewa na Mratibu wa elimu kwa umma kitengo cha
usalama barabarani Wilayani
Sengerema Coplo
Echikaka Mbozi wakati akichangia maoni
katika kipindi cha Pambazuko
kilichokuwa kikihoji Kampeni
ya pasa sauti abiria imefanikiwa kwa kiasi gani?
Akijibu hoja hiyo Coplo Echikaka Mbozi amesema kampeni hiyo imefanikiwa kwa
asilimia 75 nchini
na kuwataka abiria watoe taarifa kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani pale wanapoona dereva
amekwenda kinyume na sheria za usalama barabarani kwani kulalamika
hakutawasaidia .
Na Emmanuel Twimanye
Comments
Post a Comment