ANUSURIKA KIFO KISA PIKI PIKI          
Mtu mmoja  aliyejulikana kwa  jina la Leila  Mangi    Mwenye umri  wa    miaka 19 mkazi wa Igogo Wilayani Sengerema     amenusurika kifo baada ya kugongwa na pikipiki    mjini  sengerema  Mkoani    Mwanza.
Ajali hiyo imetokea  katika  barabara  iendayo Kamanga baada ya mwendesha Pikipiki  kupishana na gari aina ya fuso na kumgonga mtembea kwa miguu Leila Mangi   na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Akithibitisha kutokea kwa ajali   hiyo  Inspector Hamis Wembo  amewaomba waendesha vyombo vya moto kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo kusudiwa.


Jeshi la polisi limefika   eneo la tukio na kumchukua majeruhi  kisha  kumpeleka katika Hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa   ajili ya kupatiwa matibabu.
Na Said Mahera

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA