WANAFUNZI 2,262VYUMBA VYA MADARASA SITA SHULE
YA MSINGI MNADANI.
Kutokana na kuwepo kwa
changamoto ya uhaba wa vyumba vya
madarasa katika shule ya
msingi mnadani iliyopo
kata ya Nyampulukano
wilayani sengerema tatizo hilo
limeanza kupatiwa
ufumbuzi .
Hayo yamebainishwa
na Afisa mtendaji
wa kata ya Nyampulukano BI. SOPHIA
MANYILIZU na kusema kuwa shule
ya msingi mnadani
ina jumla ya wanafunzi
2262 huku ikiwa na vyumba
vya madasa sita
hali ambayo inapelekea
baadhi ya wanafunzi kushindwa kufanya
vizuri katika masomo yao.
Hata hivyo
diwani wa kata
ya Nyampulukano Mh,Emmanuel
Zacharia Mnwanizi amesema
wanahitaji kuongeza
madarasa manne ili
kupunguza adha iliyopo ya
uhaba wa vyumba
vya madarasa katika shule
hiyo.
Aidha diwani
mnwanizi amewaomba wadau
mbalimbali kujitolea nguvu
zao ili kuhakikisha
kwamba ujenzi wa
vyumba vya madarsa unaanza
mara moja.
Na Enosy Mashiba.
Comments
Post a Comment