JAMII YATAKIWA KUIMALISHA ULINZI

Jamii imetakiwa kuimalisha ulinzi katika maeneo yao ili kupambana na vitendo vya kihalifu vinavyoendelea kujitokeza katika maeneo mengi, kwani suala la ulinzi ni wajibu wa kila mtu.
Taarifa  na  Mwandishi  wetu  MICHAEL MGOZI.
Hayo yamebainishwa na Afisa mtendaji wa kata ya Ibisabageni Bwn,Adam  Salum  wakati akizungumza na Radio Sengerema Ofsini kwake.

Bwn, Adam ameongeza kuwa jamii inapaswa kutambua suala la ulinzi na kulisimamia vyema,kwani ni wajibu wao kuwafichua wahalifu wanaoishi katika maeneo yao.



Aidha Afisa Mtendaji huyo amewataka wanachi kuwabaini wahalifu mapema kabla hawajafanya uhalifu na kuacha tabia ya kusubiri tukio la kihalifu pindi linapotokea ndipo wanaanza kuimalisha ulinzi. 
Na Michael Mgozi.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA