UCHAFUZI KANDO KANDO MWA ZIWA VICTORIA
Wananchi
wa Kijiji cha Nyakaliro Kata ya Nyakaliro Halimashauri ya Buchosa Wilayani
Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kuacha kukata miti kandokando mwa ziwa victoria
ili kulinda mazalia ya samaki,na kuepusha mmomonyoko wa udongo unaoweza
kujitokeza.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyakaliro Bwn MAGAKA SITTA,wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake.
Bwn
SITTA Amesema kuwa ,wakati mwingine samaki huzalia kandokando ya ziwa,wanapokata
miti na sehemu hiyo kubaki wazi, hali hiyo huchangia kuondoa viumbe hai
wanaokuwa na makazi katika maeneo hayo.
Hata
hivyo ameongeza kuwa zipo sheria
ndogondogo walizo weka ili kulinda vyanzo vya maji pamoja na uhifadhi wa
mazingira kandokando mwa vyanzo vya maji na ziwa kwa ujumla.
misitu.
Na Michael Mgozi
Comments
Post a Comment