KATIZO LA MAJI LAWATESA WAKAZI WA SENGEREMA
Emmanuel Kipole |
Kutokana na kuwepo kwa tatizo
la kukatika kwa huduma ya maji mjini Sengerema kwa takribani wiki mbili sasa bila taarifa yoyote
kutoka mamlaka husika ya
maji, Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Emmanuel Kipole ametolea ufafanuzi wa kina suala hilo .
Akitilitolea ufafanuzi
jambo hilo mkuu wa wilaya
ya Sengerema ameiambia Radio Sengerema kuwa
tatizo hilo limetokana na deni waliokuwa wakidaiwa siku za nyuma na
shirika la umeme Tanzania (TANESCO) zaidi ya milioni 200 hali iliyopekea kukatiwa
umeme katika chanzo cha maji cha Nyamazugo.
Mh,KIPOLE Amesema juhudi zinafanyika ili kutatua tatizo hilo huku akiwaomba radhi wananchi kwa adha wanayoipata ya ukosefu wa
huduma ya maji.
Aidha amewaomba
wananchi waendelee kulipa bili ya maji ili
kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza.
Na Anna Elias
Comments
Post a Comment