WANANCHI WAJENGEWA DARAJA
Wananchi wamepongeza juhudi za serikali kwa kujenga daraja la Bulunga katika kijiji cha Nyamililo kata ya
Kasungamile wilayani Sengerema na kumaliza
kero ya muda mrefu ya kuvuka mto huo.
Wakizungumza na Radio Sengerema
kijijini hapo wamesema pamoja
na pongezi hizo
wameitaka Serikali kuboresha miundo mbinu ya barabara hiyo kutoka
Nyamililo kwenda Bulunga ambalo ni bovu
na halipitiki.
Naye Diwani wa kata ya Kasungamile mh: Julias
Ndekeja amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali ikijiandaa
kukarabati barabara hiyo.
Kukamilika kwa daraja la Nyamililo kwenda Bulunga
kumewafanya wananchi kuwa na matumaini makubwa na juhudi za serikali katika
utekelezaji wa ahadi zake.
Na Charles Sungura
Comments
Post a Comment