HUDUMA YA MAJI YAREJEA SENGEREMA
Shangwe na ndelemo
zimetawala Kwa Wananchi Wilayani
Sengerema baada ya kurejea huduma ya maji
iliyokuwa imekatika kwa takribani wiki mbili
sasa.
Wakiongea na Radio Sengerema wananchi hao wamesema maji yameanza kutoka usiku wa kuanzia leo huku
wakisema imekuwa shangwe kwao kwani walikuwa wakihofia kupatwa na magonjwa ya
mlipuko na kushukuru uongozi wa wilaya
ya Sengerema kwa jitihada za kurejesha huduma hiyo muhimu.
Hata hivyo pamoja na
pongezi hizo wananchi hao wameomba uongozi wa halmashauri kuendelea kufuatilia
deni hilo kama alivyosema mkuu wa wilaya
Mh.Emmanuel Kipole ili katizo la maji lisijirudie tena.
Na Anna Elias
Comments
Post a Comment