ELIMU BURE ISIMAMIWE IPASAVYO
Kutokana na serikali
kutumia zaidi ya shillingi bilion 18
kugharamia utekelezaji wa sera ya elimu
bure viongozi wa ngazi ya kata katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema
wametakiwa kusimamia na kuhakikisha
wanafunzi wote waliohitmu elimu ya msingi wanajiunga na masomo ya sekondari pindi watakapochaguliwa.
Hayo yamesemwa na
katibu tawala wa wilaya ya Sengerema Bwn,
Aron Laiza amesema serikali ngazi ya
kata,kijiji inatakiwa kusimamia
wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Pia ameongeza kuwa kwa mzazi yeyote atakabainika kumzuia mtoto
kwenda shule hatua kali zitachukuliwa na
viongozi dhidi yake.
Hata hivyo utekelezaji
wa sera ya elimu bure unalenga kutoa fursa ya elimu kwa watoto wote nchini ili
kila mmoja aweze kupata haki yake ya msingi ya elimu.
Na Deborah Maisa
Comments
Post a Comment