WANANCHI WAJITOLEA KUKARABATI BARABARA ZA MITAA
Wananchi wa mtaa
wa Kilabela kata
ya Mwabaluhi wilayani
Sengerema mkoani Mwanza, wameamua kushirikiana kwa pamoja kukarabati
barabara za mtaa huo ili kupunguza adha wanayoipata wakati kusafirisha mazao
pamoja na wagonjwa.
Wananchi hao wameeleza
kuwa ushirikiano huo umesaidia kuwepo
kwa barabara za
kutosha zinazopitika kwa urahisi hali ambayo wameeleza kuwa inasaidia kuongeza
maendeleo katika mtaa huo.
Akizungumza na Radio
Sengerema ofisini
kwake , Mwenyekiti wa mtaa
huo bw, Samweli Macheni Nzungu amesema
wananchi wake wanaonyesha mshikamano
mzuri wa shughuli mbali mbali za
kimaendeleo.
Sanjari na
hayo bw, Nzungu amewasihi wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano ili wasonge mbele zaidi.
Na Thobias Ngubila
Comments
Post a Comment