WITO WA JAMII
Wazazi
wametakiwa kuwalea watoto kiroho na kimwili ili wawe na tabia njema ya
kumpendeza mwenyezi mungu katika maisha yao.
Wito huo umetolewa na
mchungaji wa kanisa la Africa inland church of Tanzania (A.I.C.T) Pastoreti ya
Nyamililo Kata ya kasungamile wilayani Sengerema mkoani Mwanza Mchungaji Adamu Loke Mabindo kwenye sherehe ya
kukabidhi biblia na vyeti kwa watoto waliohitimu mafunzo ya neno la mungu.
Mchungaji Mabindo amesema msingi imara wa maisha
kwa watoto ni kuwafundisha neno la mungu ili wamjue mungu na kisha elimu ya
dunia ambayo itawasaidia kimwili.
Aidha mchungaji huyo
ameyashukuru mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mwanza children Action Network
na shirika la samalatans Purse kitengo cha O.C.C kwa kutoa biblia na vyeti kwa
watoto.
Mchungaji Mabindo ameahidi kuendelea kushirikiana mashirika
hayo ili kuboresha darasa la watoto.
Mchungaji amewaomba
wananchi kuungana kwa pamoja katika malezi ya watoto kwakuwa jukumu la kuwalea
watoto katika maadili mema inawahusu wote hivyo umoja na ushirikiano kutenda
kazi ya mungu ni muhimu sana.
Na Charles Sungura
Comments
Post a Comment