WAFANYAUSAFI WASITISHA MGOMO WAO WALIPWA STAHIKI ZAO SENGEREMA
Hatimae vizimba vya taka vilivyokuwa vimejaa kwa zaidi ya wiki mbili bila kuondolewa taka na
kusababisha kero kwa wakazi wa mji wa sengerema,vimeanza
kuondolewa baada ya wahusika kumaliza mgomo wao.
Akizungumza na Radio sengerema
meneja wa kampuni ya Stumarcot Company Limited Bwn CHARLES NGAIZA, amesema,uchafu
ulikuwa umejaa kutokana na mgomo wa wafanyakazi wa kampuni
hiyo.
Aidha Bwn NGAIZA
ameongeza kuwa,toka tarehe moja mwezi huu, wafanyakazi walikuwa wamegoma
na kusababisha mlundikano wa taka
katika vizimba vyote vya mji wa sengerema.
Sanjari na hayo kiongozi huyo amesema,watatumia wiki moja kuhakikisha
wanamaliza kuondoa uchafu huo, na kwa sasa wameanzia madampo
yaliyopo katikati mwa mji wa sengerema hususani maeneo
ya kituo cha mabasi sengerema,
Na Michael Mgozi
Comments
Post a Comment