WAFANYA USAFI WAGOMA MJINI SENGEREMA
Wafanyausafi
mjini Sengerema wamegoma kuendelea
kufanya usafi kwa takribani
wiki mbili sasa kutokana na kutolipwa
stahiki zao kwa muda mrefu.
Wafanyausafi hao wamedai
kuwa kumekuwa na
tatizo la kutopewa
mishahara yao kwa
wakati hali ambayo
imekuwa ikikwamisha zoezi
zima la usafishaji
wa mji kwa
wakati.
Akijibu madai hayo
Meneja wa kampuni
ya Stumarcot
Company Limited amekiri
kuwepo kwa hali hiyo
na kuongeza kuwa
madai ya mishahara
kwa wafanyausafi hao yamechukuwa muda
mrefu na kwamba suala hilo wameanza kulitatua.
Aidha tatizo
hilo la ktolipwa stahiki zao kwa
wakati limesababisha wafanyausafi kukata
tamaa kuendelea na
kazi hiyo kwa
kuhofia kukosa maslahi yao.
Na Thobias Ngubila
Comments
Post a Comment