MKUU WA SHULE ALIYEJINYONGA AZIKWA
Mwili wa aliyekuwa mkuu wa shule ya Sekondari Migukulama iliyopo
katika kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema hatimaye
umezikwa nyumbani kwao katika kata ya Kasisa halmashauri ya Buchosa.
Mazishi
hayo yameongozwa na Mkurugezi Mtendaji wa halmashauri ya Buchosa Bwana Crispin
Luanda ambaye amewakilishwa na Afisa elimu shule za Msingi Bi, Magreti Kapolesya.
Bi.
Kapolesya akitoa salamu za rambirambi kwa wana
familia na wanachi wa kijiji hicho amesema serikali imepoteza nguvu kazi kwani bado umli wake ulihitajika kulitumikia
taifa
Ikumbukwe
kuwa mkuu wa shule ya sekondari Migukulama Benedictor Rweikiza (45) Octoba 9 mwaka huu
alikutwa akiwa amefariki dunia
kwakujinyonga kwa kutumia kamba nyumbani kwake katika mtaa wa kilabela
kata ya Nyatukala wilayani Sengerema.
Mazishi
hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo watumishi wa halmashauri ya
Buchosa,Mbunge wa jimbo la Buchosa,wakuu wa shule jirani madiwani,walimu na
wanafunzi wa shule ya sekondari Migukulama.
Na Katemi Lenatus
Comments
Post a Comment