UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Jamii imetakiwa kutunza mazingira kwa kuhakikisha
kila kaya inakuwa na choo cha kudumu ili kuepusha uharibifu wa mazingira katika
maeneo yao.
Hayo yamesemwa na afisa
afya wa kata ya Igalula Bwn;Emmanuel
Saguda katika kikao na wananchi wa kijiji cha Nyasigu
kata ya Igalula wilayani Sengerema, ambapo amesema kumekuwepo na tabia ya
baadhi watu kusubiria ukaguzi ndipo wanatengeneza vyoo vya muda ili kujikinga
na ukaguzi huo.
Kwa upande wake Diwani
wa kata ya Igalula Mh, Onesmo Mussa
Mashiri amewaomba wananchi wote kunzingatia yanayo semwa na wataalamu kwa
kutunza mazingira.
Hata hivyo maeneo
mengi ya vijijini yamekuwa yakikabiliwa
na changamoto ya ukataji miti ovyo, uhaba wa vyoo hivyo kupelekea wananchi
kujisaidia vichakani jambo ambalo siyo salama kwa afya zao.
Comments
Post a Comment