WANANCHI WABORESHA HUDUMA ZA MAJI
Wananchi   wa    Kitongoji  cha  Kanyamwanza  kata  ya Mwabaluhi  wilaya ya sengerema mkoani mwanza  wamepongezwa       kwa  juhudi     za   kuboresha huduma ya maji  kwa kuvuta mabomba ya maji   katika  kitongoji    chao. 

Pongezo hizo   zimetolewa  na     mwenyekiti wa kitongoji cha kanyamwanza bwana INNOCENT SEGEREDI  wakati  akizungumza  na  wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji hicho  ambapo   amewambia wananchi wake hawana budi kujipongeza kwa juhudi walizozifanya za kusogeza maji  karibu na makazi yao.
Bwana INNOCENT amewaasa wananchi wake wanaohitaji kuvuta maji waweze kuchangia kiasi cha fedha walichokubaliana katika mitaa yao ili waweze kupata maji na wasitegemee  kula  kwa   nguvu za   wenzao.

Pamoja na hayo mwenyekiti huyo  amewaomba wakazi  wa eneo hilo   waendelee kuyatunza mazingira yanayowazunguka hasa kwa kipindi hiki cha mvua.
NA ENOCK  MAKALA

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA