UVAMIZI WAFANYIKA SENGEREMA
Kutokana na
Kudhibitiwa vikali matukio
mbalimbali ya uporaji wilayani
Sengerema Mkoani Mwanza, kwa
sasa yameibuka tena kwa sura mpya katika kata ya
Mwabaluhi kitongoji cha Kanyamwanza
wilayani Sengerema, baada ya
kuvamiwa familia ya Mzee Joseph Maganga
na kuiba vitu mbalimbali.
Tukio hilo
limetokea katika eneo hilo ambapo watu wanaosadikiwa kuwa
ni majambazi hao wamefanikiwa
kupora vitu ikiwemo frati skilini
1 Deki 1 na simu 3 za mkononi
vyenye Thamani ya shilingi milioni moja na laki nne na nusu, na
kutokomea navyo kusikojulikana .
Imeelezwa kuwa
watu hao wametumia ufunguo maarufu kama masta kii kufunguwa mlango wa geti na baada ya
kufungua geti hilo wakapiga
fatuma mlango wa ndani na kufunguka ndipo walipoingia na kuanza zoezi la
upekuzi na kubeba mali hizo.
Kwaupande wake mwenye
kiti wa mtaa wa eneo la Kanyamwanza
kulikofanyika wizi huo Bw,Peter
Mlashani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kuongeza kuwa wanatakiwa kuunda mikakati mathubuti ya kupambana na watu hao kwa
ushirikiano na jeshi la polisi.
Sanjari na hayo
Bw,Mlashani ameeleza kuwa kutokana na mtililiko wa matukio hayo ,
inaonekana kuna wenyeji kwani siku doria
isipokuwepo kazini
matukio ya uharifu
hujitokeza mara kwa
mara.
Na Thobias Ngubila
Comments
Post a Comment