MADEREVA WANAOBEBA MISHIKAKI KUKIONA CHA MOTO
kikosi cha usalama
barabarani kimewatangazia vita madereva
wanaobeba abiria zaidi ya mmoja
hususani wanaosafirisha abiria kwenda
vijijini.
Vita hiyo imetangazwa
na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Inspector Hamis Wembo wakati
alipokuwa akiongea na Radio Sengerema amesema
kwa maeneo ya vijijini wameelekeza majeshi ili kuhakikisha badereva
ambao hawatii sheria bila shuruti
wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Inspector
Hamis Wembo ameeleza mikakati ambayo
kikosi cha usalama barabarani watakayoitumia ili kuakikisha wanawakamata
waendesha bodaboda ambao watakaobeba abiria zaidi ya mmoja.
Katika hatua nyingine Inspector wembo amewaomba madereva kuzingatia uvaaji wa kofia
ngumu kwa abiria
kwani ni kwaajiri ya usalama wa
maisha yao.
Na Said Mahera
Comments
Post a Comment