Posts

Showing posts from January, 2018

AHUKUMIWA KWENDA JELA MWAKA 1 KWA WIZI WA DAWA SENGEREMA

Image
Mahakama   ya wilaya   ya  Sengerema  Mkoani  mwanza  imemhukumu   mtu  mmoja  kulipa   faini  kwa  makosa  matano  ,ambapo  kosa  la  kwanza hadi  tatu     atalipa   shilingi  laki   nne  au  kwenda  jela  mwaka  mmoja  kwa kila   kosa  na  kosa la nne   na  la  tano    atalipa  faini   ya  shilingi   laki   tano   au  kwenda  jela  miaka  miwili  kwa  kila   kosa. Akisoma   mashitaka   hayo  yanayomkabili  mbele  ya  hakimu   wa  mahakama   hiyo  BI   MONIKA   NDYEKOBORA  ,mwendesha  mashitaka  wa  jeshi  la  polisi   inspecta   MARTHA  SLIVESTA   amemtaja  mshitakiwa   kuwa   ni  SHABANI  IBLAHIMU  mkazi  wa  ibisabageni   wilayani   hapa. INSPECTA   MARTHA  amesema  kuwa  mshitakiwa  anashitakiwa  kwa  makosa  matano  ambapo  kosa  la  kwanza  ni   kukutwa  na     dawa    kwenye  kibanda       ambazo  hazijasajiliwa ,kinyume   na   kifungu  namba  18   kifungu  kidogo   cha  kwanza  cha  sheria  ya  chakula  na  dawa  ambapo  mnamo  novemba  27   mwaka  jana  majira  ya

ELIMU YA MATUMIZI YA ZEBRA CROSS YATOLEWA KWA WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO NA WATEMBEA KWA MIGUU SENGEREMA

Image
Jeshi la polisi  kitengo cha usalama barabarani wilayani Sengerema Mkoani Mwanza  limewataka waendesha vyombo  vya  moto  pamoja  na waendesha baiskeli kuzingatia alama za  barabarani ili kuwapa fursa     watembea kwa miguu  kuvuka barabani . Mratibu  Elimu kwa umma kitengo cha usalama barabarani  Coplo  Echika  Mbozi  ameyasema  hayo wakati akiongea na  Radio  Sengerema   na kusema  kuwa  wananchi wote wana haki ya kutumia barabara kwani ni mali ya   umma . Pia ameongeza kuwa hadi sasa wanaendelea kutoa elimu kwa jamii  ili kutambua alama zilizowekwa barabarani na sheria zake kwani wengi wao hawajajua matumizi yake pale wanapoona chombo chochote CHA Moto  kimesimama sehemu  husika ya kivuko cha watembea kwa miguu. Kwa upande wao baadhi ya wananchi wilaya sengerema wamepongeza juhudi zinazo endelea kufanywa na kitengo cha usalama barabarani kwani kumekuwepo na unyanyasaji kwa watembea kwa miguu pale wanapotaka  kuvuka  barabara.   Sanjari na hayo Mbozi amewatak

WIKI YA SHERIA, WANANCHI WILAYANI SENGEREMA WAPONGEZWA

Image
Hakimu   wa  mahakama  ya  wilaya  ya  Sengerema  mkoani   mwanza  BI ,  MONIKA   NDYEKOBORA,amewashukuru  wananchi  kwa  kujitokeza  kwa  wingi  kufika   mahakamani   hapo  kwa  lengo  la kujifunza   mambo  mbalimbali  ya  kisheria  ikiwemo  matumizi   ya  tehama. Ameyasema  hayo  alipokuwa  akiongea   na  Radio  Sengerem  ofisini   kwake ,ambapo  amesema kuwa,  hapo   awali    wananchi  walikuwa  na  mwamko  mdogo  katika  maadhimisho   ya  wiki   ya  sheria  nchini, na kuongeza  kuwa  katika  maadhimisho  ya  mwaka  huu  wananchi wameonyesha  mwamko  mkubwa   katika   kuadhimisha    wiki  ya  sheria.  Katika  maadhimisho  hayo  yaliyozinduliwa  katika  viwanja  vya  mnadani  wilayani  Sengerema  Januari   28  mwaka huu,  wananchi wamefika  katika  maeneo  hayo  na  kupatiwa  elimu  mbalimbali   na  watalamu   wa  sheria,ambapo  zoezi  la  kutoa  elimu   ya  sheria  limeendelea  katika  mahakama  ambapo   wananchi  wanaendelea  kufika  katika  madawati  mbalimbali   na  

GHARA LA KUHIFADHIA CHAKULA LAGEUKA KUWA OFISI YA KATA YA IBONDO

Image
Viongozi wa serikali ya kata ya Ibondo wilayani Sengerema wanakabiliwa na ukosefu wa ofisi ya kata hali inayowalazimu kutumia   ghara   ambalo   hutumika kutunzia zao la pamba katika     kuendesha         shughuli za kiofisi. Hayo yamebainika kwenye kikao cha mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Sengerema (CCM) Bwn Mark Augustine Makoye wakati alipokuwa akisomewa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ccm na afisa mtendaji wa kata hiyo bi Happyphania Damian . Kwa upande wake diwani wa kata ya Ibondo Mathias Mashauri amesema kukosekana kwa ofisi ya kata kumepelekea kukwamisha shughuli za kijamii katika kata hiyo. Licha ya   kutokuwepo   kwa ofisi ya kata Afisa Mtendaji   ametoa   mikakati waliojiwekea huku diwani akiwaomba wananchi kujitoa ili kuhakikisha malengo yao yanatimia. Nae mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm amewaunga mkono kwa kuchangia awamu 9 za mawe ikiwa awamu 4 ni kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya kata na awamu 5 kwa ajili ya

MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA AWAOMBA RADHI WANANCHI

Image
Baada ya siku chache wananchi wa wilaya ya Sengerema kupaza kilio chao kwa viongozi juu ya kukatika ghafla kwa huduma ya maji katika mji wa sengerema.Mkuu wa wilaya ya sengerema Mh.Emanuel Kipole amewaomba radhi wananchi kwa usumbufu wanaondelea kuupata kutokana na ukosefu wa maji. Mh.Kipole ameomba radhi wakati akizungumza na Radio Sengerema ambapo amesema kuwa   katizo la maji limetokana       na deni la zamani la umeme ambalo limepelekea kukatwa kwa umeme katika chanzo cha maji na kusababisha adha hiyo kwa wananchi wa mji wa     Sengerema. Kufuatia hali hiyo,Mh. Kipole amesema kuwa wanaendelea kukabiliana na changamoto hiyo ya katizo la maji na kuweka wazi kuwa muda wowote kuanzia   januari   30 mwaka huu   huduma hiyo muhimu kwa binadamu huenda ikarejea   katika   hali   yake   ya   kawaida. Mji wa Sengerema umekumbwa na katizo la maji kwa takribani zaidi ya wiki mbili sasa,hali ambayo imepelekea baadhi ya wananchi kutumia maji ya kwenye madimbwi na mifereji yasiyo

NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Image
Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) leo Januari 30, 2018 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na mwaka jana 2016. Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde ametangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.  "Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7"  alisema Msonde  Mbali na hilo Msonde aliweza kuweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 265 wamebainika kufanya udanganyifu mbalimbali katika mitihani hiyo ambayo ilianza kufanyik

SHULE YA SEKONDARI YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA SENGEREMA

Image
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Tunyenye wilayani Sengerema Samson Peleka a mesema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto kutokamilika kwa  ujenzi wa vyumba vya madarasa  katika shule ya msingi na sekondari Tunyenye. Ameyabainisha hayo wakati akiongea na Radio Sengerema    ambapo amewataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika kukamilisha ujezi wa vyumba vya madarasa hayo   ili wanafunzi wasome katika Mazingira rafiki. Hata hivyo bwn Samsoni ameishukuru serikali kwa      mchango  wa madawati. Sanjari na hayo Afisa Mtendaji amewaomba wananchi    waendelee kutoa ushirikiano  pindi wanapohitajika na kutoa michango mbalimbali ili kuleta maendeleo katika kijiji hicho. Bwiza Boniphace

BUNGE KUANZA TENA JANUARI 30 2018

Image
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza  kesho Janauari  30 mwaka huu  na Mkoani Dodoma kwa kuanza kuapisha Wabunge wapya watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya sheria ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tisa. Hayo yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano na kuwataja wabunge hao  watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbara kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa Singida Kaskazini na    Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido. Aidha, katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 ya kiwa ya papo kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo yanatarajiwa kuulizwa siku ya Alhamisi   februari mosi. Kwa upande mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu zitawasilisha taarifa zake Bungeni hapo.

HEKARI 6 ZAHARIBIWA NA MVUA YA MAWE KIJIJI CHA TUNYENYE WILAYANI SENGEREMA

Image
Takribani hekari sita 6 za zao la pamba zimeharibiwa na mvua ya   mawe katika kijiji cha Tunyenye kata ya Kishinda wilayani Sengerema mkoani   Mwanza.     Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwn Samson Peleka   amekiri kuwepo kwa tukio hilo lililotokea hivi karibuni   na amewataja   baadhi ya wahanga watukio hilo. Aidha Afisa mtendaji huyo amewaomba wahanga hao wasubiri ushauri kutoka kwa wataalamu wa kilimo ili   kujua   nini kifanyike   juu ya mazao   yao. Nao   baadhi ya wahanga wa tukio hilo   wakiongea kwa masikitisho wamesema     mvua hiyo imeharibu zao   hilo hivyo wameiomba serikali kuwasaidia wahanga wa mvua hiyo. Bwn Samson amewaomba   wahanga   wa tukio hilo wasikate tamaa kwani serikali kupitia idara ya kilimo   ipo pamoja nao. Na ESTHER MABULA

WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO AZINDUA MASHINE YA CT-SCAN BUGANDO MWANZA

Image
Waziri wa afya Ummy Mwalimu ameahidi kuwaletea mashine ya uchunguzi ya MRI katika hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa Bugando mwaka huu.   Ameyasema hao Januari 26 wakati akifungua mashine ya  CT-scan ambayo itakua inapima magonjwa mbalimbali iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambazo zinetokana na vyanzo mbalimbali vya hospitali hiyo Aidha,Waziri Ummy ameahidi ndani ya miaka mitatu kuanzisha taasisi ya moyo ili kuweza kupunguza gharama kwa wananchi wa kanda ya ziwa na magharibi wanaopata matatizo ya moyo kwenda kuoata vipimo na matibabu kwenye taasisi ya moyo ya  JKCI ya jijini Dar es Salaam. Na Veronica  Martine.

MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA AWANYOOSHEA KIDOLE WATENDAJI WANAOKUMBATIA UVUVI HARAMU WILAYANI SENGEREMA

Image
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Emmanuel Kipole amewashukuru wananchi kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kutokomeza  uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria  wilayani hapa. Mh,Kipole amesema kuwa kutokana na elimu inayoendelea kutolewa juu ya athari za uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kuwafichua wanaojihusisha na shughuli hiyo ikiwemo baadhi yao kuzisalimisha nyavu haramu kwa hiyari. Mkuu wa wilaya ameendelea kusisitiza kuwa wilaya ya Sengerema haitawafumbia macho baadhi ya viongozi wanaoendelea kukumbatia suala hilo. Hata hivyo mkuu wa wilaya amewatoa hofu wananchi wasamalia wema wanaoendelea kutoa taarifa kuhusiana na uvuvi haramu kuwa wasiwe na hofu kuhusiana na usalama wao. Na Veronica  Martine.

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA JAJI MKUU WA TANZANIA

Image

WANANCHI WAJIMILIKISHA ENEO LA MSITU WA CHIGU WILAYANI SENGEREMA

Image
Uongozi wa kijiji cha Nyamkorechiwa kata ya Buhama halmashauri ya Buchosa umemuomba mkuu wa wilaya ya Sengerema Bwn, Emmanuel   kipole kuingilia  kati mgogoro wa mpaka wa hifadhi ya msitu wa Chigu uliopo katika kijiji hicho. Wakizungumza na Radio Sengerema wananchi wa kijiji hicho wameelezea kuwa hifadhi hiyo ya msitu ilikuwepo tangu mwaka 1994 mpaka hivi sasa eneo hilo limetoweka kutokana na baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kilimo  hali inayopelekea eneo hilo kukosekana kwa mpaka wa eneo hilo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya kijiji Bw Alex  John amekiri kuwepo kwa wananchi waliojimilikisha eneo hilo kwa ajili ya shughuli za kilimo  na kwamba  tayari  suala hilo limefikishwa kwa mkuu wa wilaya lakini bado halijapatiwa ufumbuzi. Hata hivyo mwenyekiti huyo amewaomba wananchi kuwa wavumilimu mpaka eneo hilo litakapopatiwa ufumbuzi hususani kuweka mpaka kati ya kijiji cha nyamkorechiwa na vijiji jirani. Hifadhi ya msitu Chigu ilikuwa ikitumika kwa aj

WANANCHI WATAHADHALISHWA JUU YA UTUNZAJI WA MIUNDO MBINU YA MAJI SENGEREMA

Image
Wananchi wa kijiji cha  Nyantakubwa  kata ya  Kasungamile  Wilayani  Sengerema  mkoani  Mwanza  wametakiwa  kulinda na kuitunza  miundo  mbinu  ya  maji ili iendelee kudumu  kwa muda  mrefu. Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyantakubwa Bwana Marco Matisho alipozungumza na redio Sengerema ofisini kwake Afisa  Mtendaji amesema  serikali imetumia gharama ya shilingi milioni mia nne arobaini na nne katika mradi wa maji  kutoka katika  kijiji cha  Chamabanda hadi kijiji cha  Nyantakubwa na kwamba mradi  huo umekamilika. Aidha Bwana Marco Matisho ameiomba serikali kuongeza magati ya maji ili kumaliza kabisa tatizo hilo katika kijiji cha Nyantakubwa kwa kuwa zilizowekwa sasa ni chache kutokana  hitaji la wananchi. Wananchi wa kijiji Nyantakubwa wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji hasusani wakati wa kiangazi hali iliyopelekea akina mama kuamka usiku na kutembea umbali mrefu kufuata maji. Na Charles Sungura.

TANESCO WADAIWA KUKATA HUDUMA YA MAJI SENGEREMA

Image
Wakazi wa mji wa Sengerema   mkoani Mwanza wapo hatarini kukubwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na matumizi   ya maji   machafu yatokanayo   na mvua zinazoendelea kunyesha   baada ya kutuama kwenye madibwi na mifereji   kwani miuundo mbinu ya idara ya maji haitoi maji   kwa siku kadhaa zilizopita bila kupatiwa suluhu. Wakizungumza na Radio Sengerema kwa nyakati tofauti  wananchi   wilayani hapa wamedai kuwa  wanasikitishwa na hali hiyo kwani  katika mradi wa maji huwa wanalipia bili,na katika shughuli zingine  za kifamilia wanataabika  hivyo wameiomba  serikali  kwa kushirikiana na idara ya maji  ni vyema kuwatatulia  changamoto hiyo. Akijibu madai hayo  Meneja wa mamlaka ya maji mjini Sengerema Christopher Kiwone na kueleza sababu kubwa ya kukatiwa maji ni kutokana na  deni la hapo nyuma linalodaiwa na shirika la umeme  Tanzania TENESCO  hivyo  waliokata huduma ya maji ni (TENESCO) na wala sio idara hiyo ya maji.   Aidha  mhandisi kiwone  ameongeza kuwa suala hilo tay

AFARIKI DUNIA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SHINGONI MWANZA

Image
Mtu mmoja aliefahamika kwa majina ya Elibariki Mbaga (33) mkazi wa Ibanda Nyegezi Jijini Mwanza  amekutwa akiwa amefariki dunia  akiwa na majeraha shingoni huku chanzo chake kikiwa hakifahamiki. Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mwanza Ahmedi Msangi amesema kuwa majira ya saa tatu asubuhi wananchi wamemkuta kijana huyo akiwa amefariki dunia. Kamanda Msangi ameendelea kusema kuwa Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuwabaini wahusika waliohusika na tukio hilo Aidha Kamanda Msangi amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili wawabaini waliohusika hatua kali za kinidhamu zichukuliwe. Na   Veronica  Martine                                     

MAADHIMISHO YA UGONJWA WA UKOMA DUNIANI

Image
Januari 28 2018 ni Maadhimisho ya Ugonjwa wa Ukoma Duniani. yatakuwa yamebeba kaali mbiu isemayo "Tokomeza ukoma kuzuia ulemavu miongoni mwa vijana wetu"

NYAVU HARAMU 960 ZILIZOKAMATWA ZATEKETEZWA KWA MOTO WILAYANI SENGEREMA

Image
Jumla ya nyavu haramu mia tisa sitini (960) zimeteketezwa kwa moto wilayani sengerema baada ya kukamatwa zikiwa mafichoni katika  kijiji cha Kawe kamo Kata ya kawe Kamo wilayani  Sengerema.      Akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la uchomaji wa nyavu hizo,kwa niaba ya mkuu wa wiliya Katibu Tawala wilaya ya Sengerema Bwn Alen Augustine, amesema kuwa,watu wanaoendeleza saula la uvuvi haramu waache  kwa sababu  wataendelea  kupata  hasara. Aidha Bwn Augustine amefafanua kuwa mmiliki wa nyavu hizo wamemubaini lakini walipoongea nae kwa  simu amekana kumiliki nyavu hizo, na kusema kuwa hatua za kisheria zitafuatwa ili kubaini  ukweli. Kwa  upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema Bwn Magesa  Mafuru  Bonipahace   amesema  kuwa, wamechukua hatua za kuteketeza nyavu hizo ili kukomesha vitendo vya uvuvi haramu. Na  MICHAEL      MGOZI  .

NG'OMBE 250 WAPIGWA CHAPA SENGEREMA

Image
Ng,ombe   mia  mbili na hamsini  (250)  wamepigwa  chapa   katika kijiji cha Kang’hwashi   kata ya Nyamizeze  Wilayani Sengerema . Na Emmanuel Twimanye.

SAMAKI WALIOCHINI YA KIWANGO WAENDELEA KUPIGWA MNADA SENGEREMA

Image
Samaki aina ya sangara walio chini ya kiwango wanao kadiliwa kuwa na zaidi ya tani tatu wamepigwa mnada  katika halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza kwa jumla ya shilingi milioni tatu laki saba na elfu ishirini(3,7020,000). Akizungumza na waandishi wa habari katika mnada huo,Afsa uvuvi Wilaya ya Sengerema Bwn Nestory Mmbare amesama kuwa,katika mnada huo alieshinda ni Raphael Mgeta ambae ametoa fedha hiyo. Aidha Afisa uvuvi wilayani Sengerema amefafanua kuwa,mnada huo ni wa pili kufanyika katika halmashauri hiyo, na lengo si kuingiza mapato bali ni kukomesha uvuvi haramu. Akiongea kwa niaba ya wafanyabiashara wa samaki Bwn Raphael Mgeta aliyeshinda katika mnada huo,amesama kuwa wataendelea kufanya biashara hiyo kwani sasa wanafuata vigezo na masharti ya biashara hiyo.   Hata hivyo, kutokana na misako mbalimbali inayofanywa wilayani sengerema katika kukomesha suala la uvuvi haramu, jitihada hizo zimeonekana kuzaa matunda kwani  uvuvi haramu kwa sasa umepu

AFIKISHWA KITUO CHA POLISI KISA WIZI WA KUKU SENGEREMA

Image
Mtu mmoja  mkazi wa  wilaya ya Misungwi  Mwanza Bwn. Mathias  Makoye  anashikiliwa  na  jeshi la polisi   wilayani sengerema baada ya  kufikishwa kituoni hapo na  jeshi la ulinzi na usalama maarufu kama sungusungu kwa tuhuma za wizi wa kuku mtaa wa mnadani  wilayani  humo. Wakizungumza na Radio Sengerema  mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa wamesikitishwa na kitendo hicho  hivyo kuhimiza sheria ichukue mkondo wake wenye tabia kama hiyo. Aidha mtuhumiwa huyo amekiri  kutenda kosa hilo. Kamanda mkuu sungusungu mtaa wa mnadani wilayani sengerema  Bwn paul stephano  ametoa wito kwa jamii  kuendelea kutoa ushirikiano kwa  vyombo vya dola pindi  matukio ya  viashiria vya uvunjifu wa amani yanapotokea. Hata hivyo kamada huyo ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na mali zao ili kujiepusha na wimbi kubwa la wezi. Na Esther Mabula.

AJALI YA GARI YAUA WAWILI NA KUJERUHI 8 SENGEREMA

Image
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 8 kujeruhiwa baada ya  ajali ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Kamanga eneo la Chemagati wilayani Sengerema mkoani Mwanza.   Ajali hiyo imetokea januari 22 majira ya saa tatu  asubuhi  ambapo basi la kampuni ya MKOMBOZI  lililokuwa likitoka sengerema kuelekea mwanza lenye namba za usajili   T 540 DLF na WALAWI lililiokuwa likitoka mwanza kuelekea sengerema  lenye namba za usajili T 167 CSN  ambapo chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Dereva wa basi la mkombozi aliyefahamika kwa jina moja la bwn.  Simoni  amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali  ya rufaa Bugando jijini Mwanza na  abiria mmoja wa jinsia ya kike aliyekuwa kwenye basi la walawi amefariki dunia papo hapo . Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa basi la Mkombozi pamoja na abiria mwingine wamepoteza maisha hapo hapo. Na

WATUMIA SARE ZA JESHI LA POLISI KUVAMIA WATU HUKU MTU MMOJA AKILALAMIKIWA KUTUMIA MAJINA YA VIONGOZI WA NCHI KUWANYANYASA WANANCHI.

Image
Wananchi wa kijiji cha Luchili katika kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema   wamelalamikia kitendo cha baadhi ya vijana wanaotumia sare za jeshi la polisi kuvamia watu njiani      huku   mtu mmoja akilalamikiwa kutumia majina ya viongozi wa nchi kuwanyanyasa wananchi katika kijiji hicho. Hayo yameelezwa na wananchi kwenye mkutano wa Jeshi la jadi sungungusu uliofanyika katika kijiji hapo baada ya kuwepo malalamiko ya wananchi kupigwa na kunyanyaswa na baadadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi wa kitaifa. Mheshimiwa Idama kibanzi  ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa amewatahadharisha wale wanao tumia sare za jeshi la polisi kufanya uhalifu pamoja na kutumia majina ya viongozi wa kitaifa kupiga na kuwanyanyasa raia na amewataka wananchi kuwafichua watu wanao fanya hivyo kwani kufanya hivyo  ni kosa kisheria. Kwa upande afisa mtendaji wa kata hiyo Onesmo Daud  ambaye pia amekaimu Ofisi ya Afisa Mtendaji kijij