BUNGE KUANZA TENA JANUARI 30 2018
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza kesho Janauari
30 mwaka huu na Mkoani Dodoma kwa
kuanza kuapisha Wabunge wapya watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya
sheria ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tisa.
Hayo
yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge kupitia Kitengo
cha Habari na Mawasiliano na kuwataja wabunge hao watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt.
Damas Daniel Ndumbara kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa
Singida Kaskazini na Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido.
Aidha,
katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida
yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 ya kiwa ya papo
kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo yanatarajiwa kuulizwa siku ya
Alhamisi februari mosi.
Kwa upande
mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu zitawasilisha taarifa zake Bungeni hapo.
Comments
Post a Comment