SAMAKI WALIOCHINI YA KIWANGO WAENDELEA KUPIGWA MNADA SENGEREMA
Samaki
aina ya sangara walio chini ya kiwango wanao kadiliwa kuwa na zaidi ya tani
tatu wamepigwa mnada katika halmashauri
ya Sengerema mkoani Mwanza kwa jumla ya shilingi milioni tatu laki saba na elfu
ishirini(3,7020,000).
Akizungumza
na waandishi wa habari katika mnada huo,Afsa uvuvi Wilaya ya Sengerema Bwn Nestory Mmbare amesama kuwa,katika
mnada huo alieshinda ni Raphael Mgeta ambae ametoa fedha hiyo.
Aidha
Afisa uvuvi wilayani Sengerema amefafanua kuwa,mnada huo ni wa pili kufanyika
katika halmashauri hiyo, na lengo si kuingiza mapato bali ni kukomesha uvuvi
haramu.
Akiongea
kwa niaba ya wafanyabiashara wa samaki Bwn
Raphael Mgeta aliyeshinda katika mnada huo,amesama kuwa wataendelea kufanya
biashara hiyo kwani sasa wanafuata vigezo na masharti ya biashara hiyo.
Hata
hivyo, kutokana na misako mbalimbali inayofanywa wilayani sengerema katika
kukomesha suala la uvuvi haramu, jitihada hizo zimeonekana kuzaa matunda
kwani uvuvi haramu kwa sasa umepungua.
Na Michael Mgozi.
Comments
Post a Comment