AHUKUMIWA KWENDA JELA MWAKA 1 KWA WIZI WA DAWA SENGEREMA
Mahakama ya
wilaya ya Sengerema
Mkoani mwanza imemhukumu
mtu mmoja kulipa
faini kwa makosa matano
,ambapo kosa la
kwanza hadi tatu atalipa
shilingi laki
nne au kwenda
jela mwaka mmoja
kwa kila kosa na
kosa la nne na la
tano atalipa
faini ya shilingi
laki tano au
kwenda jela miaka
miwili kwa kila
kosa.
Akisoma
mashitaka hayo yanayomkabili
mbele ya hakimu
wa mahakama hiyo
BI MONIKA NDYEKOBORA
,mwendesha mashitaka wa
jeshi la polisi
inspecta MARTHA SLIVESTA
amemtaja mshitakiwa kuwa
ni SHABANI IBLAHIMU
mkazi wa ibisabageni
wilayani hapa.
INSPECTA
MARTHA amesema kuwa
mshitakiwa anashitakiwa kwa
makosa matano ambapo
kosa la kwanza
ni kukutwa
na dawa kwenye
kibanda ambazo hazijasajiliwa ,kinyume na
kifungu namba 18
kifungu kidogo cha
kwanza cha sheria
ya chakula na
dawa ambapo mnamo
novemba 27 mwaka
jana majira ya
mchana katika maeneo
ya Ibisabageni wilayani
sengerema mkoani mwanza alikutwa na
VENASI BULUSHI ambaye
ni mkaguzi wa dawa akiwa
na wenzake alikutwa
bila ruhusa yoyote
ameiba madawa yenye
thamani ya sh, milioni sitini
laki nne na thelathini na
tano na mia
sita zikiwa
katika maeneo ya
ambayo hayajasajiliwa.
Kosa la pili kuiiba dawa ambayo
hayajasajiliwa kinyume na
kifungu namba 22
kifungu kidogo cha
kwanza A na
kifungu kidogo cha ( 3) cha sheria
ya chakula na
dawa TFDA ya
mwaka 2003,kuwa mnamo
tarehe ,muda na maeneo tajwa
mshitakiwa alikutwa akiwa
ametunza bidhaa za dawa yenye
thamani ya sh,milioni mbili
laki tano na
elfu ishirini na
moja ,ambapo bidhaa hizo
za dawa hazikusajiliwa.
Kosa la tatu
kutunza bidhaa za dawa bila leseni
au kibali kinyume
na kifungu namba
22 kifungu kidogo
cha kwanza na
kifungu kidogo cha
pili ( C) na kifungu kidogo
cha tatu kuwa
mnamo tarehe ,muda na maeneo
tajwa mshitakiwa alikutwa
akiwa ametunza bidhaa
ya dawa zenye thamani ya
sh,milioni nane na elfu
kumi na nne na
mia tano bila leseni
au kibali toka
TFDA.
Kosa la nne kukutwa
na dawa isivyo halali kinyume na
kifungu namba 76 kifungu
kidogo cha kwanza
na kifungu kidogo
cha pili cha
sheria ya TFDA ambapo
alikutwa na dawa isivyo
halali zenye thamani
ya sh, laki tatu
na nusu.
Na kosa
la tano kumiliki vifaa tiba
isivyo halali kinyume na
kifungu namba 76
kifungu kidogo cha
kwanza , alikutwa akimiliki dawa zenye thamani
ya sh,milioni arobaini na
tisa laki tano
na thelathini na
mia moja isivyo
halali.
Aidha
mtuhumiwa amekiri kutenda
makosa hayo matano
aliyoshitakiwa nayo,na mahakama
kumtia hatiani kwa makosa
hayo na kuhukumiwa kosa
la 1,2,3 shilingi laki
nne au kwenda
jela mwaka mmoja
kwa kila kosa na
kosa la 4,na 5 kulipa faini
ya shilingi laki
tano au kwenda
jela miaka miwili
kwa kila kosa.
Pia na madawa
ambayo hayajasajiriwa yataifishwe
kwa mujibu wa
kifungu namba 83
cha sheria ya
TFDA na dawa zisizofaa
ziteketezwe kwa usimamizi
wa TFDA.
Hata
hivyo mshitakiwa alilipa
faini hiyo ya
makosa yote matano
na hivyo mahakama
kumwachia huru.
Na,Joyce Rollingstone.
Comments
Post a Comment