WIKI YA SHERIA, WANANCHI WILAYANI SENGEREMA WAPONGEZWA

Hakimu   wa  mahakama  ya  wilaya  ya  Sengerema  mkoani   mwanza  BI ,  MONIKA   NDYEKOBORA,amewashukuru  wananchi  kwa  kujitokeza  kwa  wingi  kufika   mahakamani   hapo  kwa  lengo  la kujifunza   mambo  mbalimbali  ya  kisheria  ikiwemo  matumizi   ya  tehama.

Ameyasema  hayo  alipokuwa  akiongea   na  Radio  Sengerem  ofisini   kwake ,ambapo  amesema kuwa,  hapo   awali    wananchi  walikuwa  na  mwamko  mdogo  katika  maadhimisho   ya  wiki   ya  sheria  nchini, na kuongeza  kuwa  katika  maadhimisho  ya  mwaka  huu  wananchi wameonyesha  mwamko  mkubwa   katika   kuadhimisha    wiki  ya  sheria.

 Katika  maadhimisho  hayo  yaliyozinduliwa  katika  viwanja  vya  mnadani  wilayani  Sengerema  Januari   28  mwaka huu,  wananchi wamefika  katika  maeneo  hayo  na  kupatiwa  elimu  mbalimbali   na  watalamu   wa  sheria,ambapo  zoezi  la  kutoa  elimu   ya  sheria  limeendelea  katika  mahakama  ambapo   wananchi  wanaendelea  kufika  katika  madawati  mbalimbali   na   kupatiwa  huduma za  kisheria.

Kwa  upande  wao   baadhi  ya  wananchi   wameishukuru   mahakama kwa  kuonyesha  ushirikiano   mkubwa  kwa  wananchi  waliofika   katika   maeneo   ya   mahakama  ili  kujua  matumizi   ya  Tehama  kwa  upande   wa  mahakama  jinsi  inavyotumika  kutoa  haki  kwa  wakati   kwa  kuzingatia  maadili.

Ikumbukwe   kuwa  siku  ya  sheria  nchini,huadhimishwa  kila  mwaka    ambapo  maadhimisho  hayo   kwa mwaka huu   yanatarajiwa  kufikia   kilele   chake februari  mosi  mwaka  huu.

Na,Joyce Rollingstone.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA