NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Baraza la
Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na
Maarifa (QT) leo Januari 30, 2018 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla
umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na mwaka jana 2016.
Katibu
Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde ametangaza matokeo hayo leo jijini Dar es
Salaam na kusema ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha
na matokeo ya mwaka jana.
"Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09% kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7" alisema Msonde
Mbali na
hilo Msonde aliweza kuweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 265 wamebainika kufanya
udanganyifu mbalimbali katika mitihani hiyo ambayo ilianza kufanyika Oktoba 30,
2016 mpaka Novemba 17, 2016 .
Comments
Post a Comment