WATUMIA SARE ZA JESHI LA POLISI KUVAMIA WATU HUKU MTU MMOJA AKILALAMIKIWA KUTUMIA MAJINA YA VIONGOZI WA NCHI KUWANYANYASA WANANCHI.
Wananchi
wa kijiji cha Luchili katika kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani
Sengerema wamelalamikia kitendo cha
baadhi ya vijana wanaotumia sare za jeshi la polisi kuvamia watu njiani huku mtu mmoja akilalamikiwa kutumia majina ya
viongozi wa nchi kuwanyanyasa wananchi katika kijiji hicho.
Hayo
yameelezwa na wananchi kwenye mkutano wa Jeshi la jadi sungungusu uliofanyika
katika kijiji hapo baada ya kuwepo malalamiko ya wananchi kupigwa na kunyanyaswa
na baadadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi wa kitaifa.
Mheshimiwa
Idama kibanzi ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Buchosa amewatahadharisha wale wanao tumia sare za jeshi la polisi kufanya
uhalifu pamoja na kutumia majina ya viongozi wa kitaifa kupiga na kuwanyanyasa raia
na amewataka wananchi kuwafichua watu wanao fanya hivyo kwani kufanya
hivyo ni kosa kisheria.
Kwa
upande afisa mtendaji wa kata hiyo Onesmo Daud
ambaye pia amekaimu Ofisi ya Afisa Mtendaji kijiji cha Luchili amesema Ofisi yake haijapata taarifa za uwepo
wa watu wanaodaiwa kutumia sare za jeshi
la polisi wala kutumia majina ya viongozi wa kitaifa .
Hata
hivyo Bwn, Daud amethibitisha tukio
la mtu mmoja kutaka kushambuliwa na wananchi hivi karibuni huku sababu za
kutaka kushambuliwa kwa kijana huyo zikiwa hazifahamiki.
Mkutano
wa jeshi la sungusungu umefanyika baada ya tukio la watu wanne kukamatwa na jeshi la polisi January 14 mwaka
huu wakituhumiwa kutaka kumshambulia mtu mmoja ambaye amekuwa akitaja majina ya
viongozi wakitafaifa katika kutekeleza adhima yake.
Na Katemi Lenatus.
Comments
Post a Comment