MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA AWANYOOSHEA KIDOLE WATENDAJI WANAOKUMBATIA UVUVI HARAMU WILAYANI SENGEREMA
Mkuu wa wilaya
ya Sengerema Mh,Emmanuel Kipole amewashukuru wananchi kwa kuendelea
kutoa ushirikiano katika kutokomeza
uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria
wilayani hapa.
Mh,Kipole amesema kuwa kutokana na elimu inayoendelea kutolewa juu
ya athari za uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria wananchi wamekuwa na mwitikio
mkubwa wa kuwafichua wanaojihusisha na shughuli hiyo ikiwemo baadhi yao
kuzisalimisha nyavu haramu kwa hiyari.
Mkuu wa wilaya
ameendelea kusisitiza kuwa wilaya ya Sengerema haitawafumbia macho baadhi ya
viongozi wanaoendelea kukumbatia suala hilo.
Hata hivyo
mkuu wa wilaya amewatoa hofu wananchi wasamalia wema wanaoendelea kutoa taarifa
kuhusiana na uvuvi haramu kuwa wasiwe na hofu kuhusiana na usalama wao.
Na Veronica Martine.
Comments
Post a Comment