AFIKISHWA KITUO CHA POLISI KISA WIZI WA KUKU SENGEREMA
Mtu
mmoja mkazi wa wilaya ya Misungwi Mwanza Bwn.
Mathias Makoye anashikiliwa
na jeshi la polisi wilayani sengerema baada ya kufikishwa kituoni hapo na jeshi la ulinzi na usalama maarufu kama sungusungu
kwa tuhuma za wizi wa kuku mtaa wa mnadani
wilayani humo.
Wakizungumza
na Radio Sengerema mashuhuda wa tukio
hilo wameeleza kuwa wamesikitishwa na kitendo hicho hivyo kuhimiza sheria ichukue mkondo wake wenye
tabia kama hiyo.
Aidha
mtuhumiwa huyo amekiri kutenda kosa
hilo.
Kamanda
mkuu sungusungu mtaa wa mnadani wilayani sengerema Bwn
paul stephano ametoa wito kwa
jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pindi matukio ya
viashiria vya uvunjifu wa amani yanapotokea.
Hata
hivyo kamada huyo ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na mali zao
ili kujiepusha na wimbi kubwa la wezi.
Na Esther Mabula.
Comments
Post a Comment