WANANCHI WATAHADHALISHWA JUU YA UTUNZAJI WA MIUNDO MBINU YA MAJI SENGEREMA
Wananchi
wa kijiji cha Nyantakubwa kata ya
Kasungamile Wilayani Sengerema
mkoani Mwanza wametakiwa
kulinda na kuitunza miundo mbinu
ya maji ili iendelee kudumu kwa muda
mrefu.
Hayo yamebainishwa na
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyantakubwa Bwana Marco Matisho alipozungumza na
redio Sengerema ofisini kwake
Afisa Mtendaji amesema serikali imetumia gharama ya shilingi milioni
mia nne arobaini na nne katika mradi wa maji
kutoka katika kijiji cha Chamabanda hadi kijiji cha Nyantakubwa na kwamba mradi huo umekamilika.
Aidha Bwana Marco Matisho ameiomba serikali
kuongeza magati ya maji ili kumaliza kabisa tatizo hilo katika kijiji cha
Nyantakubwa kwa kuwa zilizowekwa sasa ni chache kutokana hitaji la wananchi.
Wananchi wa kijiji
Nyantakubwa wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji hasusani wakati
wa kiangazi hali iliyopelekea akina mama kuamka usiku na kutembea umbali mrefu
kufuata maji.
Na Charles Sungura.
Comments
Post a Comment