MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA AWAOMBA RADHI WANANCHI
Baada
ya siku chache wananchi wa wilaya ya Sengerema kupaza kilio chao kwa viongozi
juu ya kukatika ghafla kwa huduma ya maji katika mji wa sengerema.Mkuu wa
wilaya ya sengerema Mh.Emanuel Kipole amewaomba radhi wananchi kwa usumbufu
wanaondelea kuupata kutokana na ukosefu wa maji.
Mh.Kipole
ameomba radhi wakati akizungumza na Radio Sengerema ambapo amesema kuwa katizo la maji limetokana na deni la zamani la umeme ambalo limepelekea
kukatwa kwa umeme katika chanzo cha maji na kusababisha adha hiyo kwa wananchi
wa mji wa Sengerema.
Kufuatia
hali hiyo,Mh. Kipole amesema kuwa wanaendelea kukabiliana na changamoto hiyo ya
katizo la maji na kuweka wazi kuwa muda wowote kuanzia januari
30 mwaka huu huduma hiyo muhimu
kwa binadamu huenda ikarejea katika hali yake ya
kawaida.
Mji
wa Sengerema umekumbwa na katizo la maji kwa takribani zaidi ya wiki mbili
sasa,hali ambayo imepelekea baadhi ya wananchi kutumia maji ya kwenye madimbwi
na mifereji yasiyo safi na salama,hali ambayo ni hatari kwa afya zao.
Tatizo
hilo la katizo la maji lisipo tatuliwa mapema huenda likapelekea kutokea kwa
mgonjwa ya mlipuko kwa wakazi wa mji wa Sengerema kutokana na kuendelea kutumia
maji yasiyo safi na salama.
Na Michael Mgozi.
Comments
Post a Comment