TANESCO WADAIWA KUKATA HUDUMA YA MAJI SENGEREMA
Wakazi
wa mji wa Sengerema mkoani Mwanza wapo
hatarini kukubwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na matumizi ya maji
machafu yatokanayo na mvua
zinazoendelea kunyesha baada ya kutuama
kwenye madibwi na mifereji kwani miuundo
mbinu ya idara ya maji haitoi maji kwa
siku kadhaa zilizopita bila kupatiwa suluhu.
Wakizungumza
na Radio Sengerema kwa nyakati tofauti
wananchi wilayani hapa wamedai
kuwa wanasikitishwa na hali hiyo kwani katika mradi wa maji huwa wanalipia bili,na
katika shughuli zingine za kifamilia
wanataabika hivyo wameiomba serikali
kwa kushirikiana na idara ya maji
ni vyema kuwatatulia changamoto
hiyo.
Akijibu
madai hayo Meneja wa mamlaka ya maji
mjini Sengerema Christopher Kiwone na kueleza sababu kubwa ya kukatiwa maji ni
kutokana na deni la hapo nyuma
linalodaiwa na shirika la umeme Tanzania
TENESCO hivyo waliokata huduma ya maji ni (TENESCO) na wala
sio idara hiyo ya maji.
Aidha mhandisi kiwone ameongeza kuwa suala hilo tayari idara ya maji wameshaliwasilisha kwenye
ngazi ya wizara ya maji kwani ndiyo inatakiwa kulipa deni hilo na siyo idara ya
maji.
Hata
hivyo meneja huyo amewaomba wananchi waendelee kulipia bili za mwezi uliopita kwani suala hilo serikali inaendelea
kulifanyia kazi na mda wowote huduma ya
maji itarejea.
Sanjari
na hayo Mhandisi kiwone amewataka wananchi waendelee kuilinda miuundo mbinu ya maji licha ya kuwa
haitoi huduma kwa sasa.
Na Esther Mabula.
Comments
Post a Comment