ELIMU YA MATUMIZI YA ZEBRA CROSS YATOLEWA KWA WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO NA WATEMBEA KWA MIGUU SENGEREMA
Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wilayani Sengerema
Mkoani Mwanza limewataka waendesha
vyombo vya moto pamoja
na waendesha baiskeli kuzingatia alama
za barabarani ili kuwapa fursa watembea
kwa miguu kuvuka barabani .
Mratibu Elimu kwa umma kitengo cha usalama barabarani Coplo Echika
Mbozi ameyasema
hayo wakati akiongea na Radio Sengerema
na kusema kuwa wananchi wote wana haki ya kutumia barabara
kwani ni mali ya umma .
Pia ameongeza kuwa hadi
sasa wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kutambua alama zilizowekwa barabarani na
sheria zake kwani wengi wao hawajajua matumizi yake pale wanapoona chombo
chochote CHA Moto kimesimama sehemu husika ya kivuko cha watembea kwa miguu.
Kwa upande wao baadhi
ya wananchi wilaya sengerema wamepongeza juhudi zinazo endelea kufanywa na
kitengo cha usalama barabarani kwani kumekuwepo na unyanyasaji kwa watembea kwa
miguu pale wanapotaka kuvuka barabara.
Sanjari na hayo Mbozi
amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani kutoa taarifa pale sheria na taratibu zitakapokiukwa ili hatua kali
za kisheria zichukuliwa dhidi ya mhusika.
Na Amina Hassan.
Comments
Post a Comment