AJALI YA GARI YAUA WAWILI NA KUJERUHI 8 SENGEREMA
Watu wawili wamefariki
dunia na wengine 8 kujeruhiwa baada ya ajali ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso katika
kijiji cha Kamanga eneo la Chemagati wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Ajali hiyo imetokea januari
22 majira ya saa tatu asubuhi ambapo basi la kampuni ya MKOMBOZI lililokuwa likitoka sengerema kuelekea mwanza
lenye namba za usajili T 540 DLF na WALAWI lililiokuwa likitoka
mwanza kuelekea sengerema lenye namba za
usajili T 167 CSN ambapo chanzo cha
ajali hiyo ni mwendo kasi.
Dereva wa basi la
mkombozi aliyefahamika kwa jina moja la bwn.
Simoni amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza na abiria mmoja wa jinsia ya kike aliyekuwa
kwenye basi la walawi amefariki dunia papo hapo .
Kamanda wa polisi mkoa
wa Mwanza kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa basi la Mkombozi pamoja na
abiria mwingine wamepoteza maisha hapo hapo.
Na Glorius Balele.
Comments
Post a Comment