SHULE YA SEKONDARI YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA SENGEREMA

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Tunyenye wilayani Sengerema Samson Peleka amesema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto kutokamilika kwa  ujenzi wa vyumba vya madarasa  katika shule ya msingi na sekondari Tunyenye.


Ameyabainisha hayo wakati akiongea na Radio Sengerema    ambapo amewataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika kukamilisha ujezi wa vyumba vya madarasa hayo   ili wanafunzi wasome katika Mazingira rafiki.

Hata hivyo bwn Samsoni ameishukuru serikali kwa      mchango  wa madawati.

Sanjari na hayo Afisa Mtendaji amewaomba wananchi    waendelee kutoa ushirikiano  pindi wanapohitajika na kutoa michango mbalimbali ili kuleta maendeleo katika kijiji hicho.
Bwiza Boniphace

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA