GHARA LA KUHIFADHIA CHAKULA LAGEUKA KUWA OFISI YA KATA YA IBONDO
Viongozi
wa serikali ya kata ya Ibondo wilayani Sengerema wanakabiliwa na ukosefu wa
ofisi ya kata hali inayowalazimu kutumia ghara
ambalo hutumika kutunzia zao la
pamba katika kuendesha
shughuli za kiofisi.
Hayo
yamebainika kwenye kikao cha mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya
Sengerema (CCM) Bwn Mark Augustine Makoye
wakati alipokuwa akisomewa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha
mapinduzi ccm na afisa mtendaji wa kata hiyo bi Happyphania Damian.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Ibondo Mathias
Mashauri amesema kukosekana kwa ofisi ya kata kumepelekea kukwamisha shughuli
za kijamii katika kata hiyo.
Licha
ya kutokuwepo kwa ofisi ya kata Afisa Mtendaji ametoa mikakati
waliojiwekea huku diwani akiwaomba wananchi kujitoa ili kuhakikisha malengo yao
yanatimia.
Nae
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm amewaunga mkono kwa kuchangia awamu 9 za
mawe ikiwa awamu 4 ni kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya kata na awamu 5 kwa ajili
ya ujenzi wa ofisi ya CCM ya kata
Hata
hivyo Mh Mark Augustene Makoye amewaomba
wananchi watakapoambiwa na viongozi wao kuchangia shughuli za kimaendeleo
wasisite kuchangia kwani maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe na serikali
haitasita kuwaunga mkono.
Na Said Mahera
Comments
Post a Comment