WANANCHI WAJIMILIKISHA ENEO LA MSITU WA CHIGU WILAYANI SENGEREMA
Uongozi
wa kijiji cha Nyamkorechiwa kata ya
Buhama halmashauri ya Buchosa umemuomba mkuu wa wilaya ya Sengerema Bwn, Emmanuel
kipole kuingilia kati mgogoro
wa mpaka wa hifadhi ya msitu wa Chigu uliopo katika kijiji hicho.
Wakizungumza
na Radio Sengerema wananchi wa kijiji hicho wameelezea kuwa hifadhi hiyo ya
msitu ilikuwepo tangu mwaka 1994 mpaka hivi sasa eneo hilo limetoweka kutokana
na baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kilimo hali inayopelekea eneo hilo kukosekana kwa
mpaka wa eneo hilo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa serikali ya kijiji Bw Alex John amekiri kuwepo
kwa wananchi waliojimilikisha eneo hilo kwa ajili ya shughuli za kilimo na kwamba
tayari suala hilo limefikishwa
kwa mkuu wa wilaya lakini bado halijapatiwa ufumbuzi.
Hata
hivyo mwenyekiti huyo amewaomba wananchi kuwa wavumilimu mpaka eneo hilo
litakapopatiwa ufumbuzi hususani kuweka mpaka kati ya kijiji cha nyamkorechiwa
na vijiji jirani.
Hifadhi
ya msitu Chigu ilikuwa ikitumika kwa ajili ya malisho ya mifugo na shughuli za
kiserikali.
Na Tumain John.
Comments
Post a Comment